Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma
Picha kwa niaba ya blogu la bongo ndiyo home |
Mkuu wetu wa mkoa wa Mtwara amepatiwa nishani ya Utumishi uliotukuka kwa kanisa na jamii. Hii ni habari njema kwa mkoa wa mtwar. Mchango wake huo ni ule alioutoa kwa taifa hususan kwa mkoa wa kigoma. Kwa Mtwara ni furaha kubwa kwa kuwa tumepata mkuu ambaye ana sifa za uchapaji kazi. Ndugu mkuu wa mkoa endelea na moyo huo ili utakapokamilisha shughuli zako nasi wanaMtwara tutakupatia nishani nyingine bila shaka. Kwa sasa hongera sana kwa mchango wako.
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict wa XVI amemtunuku nishani ya Mtakatifu Gregory Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia kwa utumishi uliotukuka kwa kanisa na jamii.
Nishani hiyo ilikabidhiwa kwa Simbakalia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa karibu miaka sita, na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Protas Rugambwa kwa niaba ya Papa katika misa ya Ibada ya Krismasi iliyofanyika kwenye Kanisa la Bikira Maria mshindaji mjini Kigoma.
Simbakalia alitiririkwa na machozi wakati akikabidhiwa nishani hiyo kutokana na kutoamini kile anachokiona hali iliyofanya kanisa kuzizima kwa hali hiyo katika tuzo hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa kwa muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma tangu kuanzishwa kwake.