Tafakuri ya leo;
Uchambuzi wa kitabu kiitwacho WHO WILL CRY WHEN YOU DIE Na Robin Sharma.
Habari mpendwa msomaji
wa makala hizi naamini unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku,basi leo
nimetamani tupate muendelezo na tuendelee kujifunza katika mambo mazuri ambayo
mwandishi Robin Sharma ametushirikisha katika kitabu chake cha Who will cry
when you die.Kwenye makala iliyopita tulipata kuona mambo tisa kati ya 101 basi
leo tuendelee kujifunza mambo mengine machache ambayo tukiyatenda hakika
itakuwa ni faida kwetu na kwa vizazi vijavyo.
Jambo la kwanza ni
kuishi kinyenyekevu(be humble),mtu yeyote aishiye maisha ya unyenyekevu kwanza
kabisa huwa tayari kujifunza kwa wengine lakini pia hujijengea mahusiano bora
na watu wanaomzunguka na jamii kwa ujumla,hivyo unyenyekevu ni silaha kubwa
sana ya kuishi nayo,jamii itakuwa ikijifunza kwako na itamani kuendelea kuwa na
wewe na hata siku ukifa itakukumbuka na kukulilia sana.
Jitoe kubeba hatari
kubwa(risks).Siku zote mtu aliyeradhi kubeba hatari kubwa huwa ndiye anayepata
matokeo makubwa,hivyo basi usiwe muoga kubeba hatari kubwa katika maisha yako
binafsi,jamii na hata kwa taifa kwa ujumla.
Acha kuwa na hofu na
vitu ambavyo huna uwezo wa kuvibadilisha.Hii pia ni moja ya changamoto kubwa
sana watu wanayokutana nayo katika maisha yao ya kila siku,unakuta mtu anawaza
mambo makubwa na ya hatari ambayo hayawezi kutokea ama hana uwezo nao wa
kuyabadilisha,ndugu yangu acha kuwaza vitu vilivyo nje ya uwezo wako,maana
hatari yake ni kuwa utajikuta ukipoteza nishati nyingi huku ukipata matokeo
kidogo na hii ni hasara.
Penda kazi yako.Kuna
msemo unasema "kazi mbaya ukiwa nayo",hii huonyesha ni jinsi gani
watu hudharau kazi zao pindi pale wanapokuwa wakizifanya na kujiona kama wao ni
watu duni tofauti na wengine,lakini dhana hii ni potofu,unachotakiwa ni
kuipenda kazi yako hata kama ni ndogo kiasi gani au wewe unaiona ni dunia kiasi
gani utakapoipenda kazi yako utaifanya kwa ufanisi na hata wale uwapao huduma
yako watavutiwa sana na watakukumbuka sana hata siku ukiwa haupo tena duniani.
Pia tuwapo katika
shughuli zetu za kazi baada ya kumaliza wakati mwingine hujikuta tukiwa
tumechoka na wenye mawazo mengi sana,lakini unachotakiwa kufanya ni kutafuta
namna ya kuondoa hayo mawazo ya kazi kabla haujafika kwenye mlango wa
nyumbani,kumbuka kwamba na familia nayo inatamani uwepo wako hivyo unapofika
huku ukiwa na mawazo hutakuwa na uwezo wa kushirikiana vyema na familia yako na
hii hupelekea kupunguza mahusiano mazuri na familia yako.Unaweza sikiliza
miziki tulivu hii itakusaidia kukuweka sawa kiakili kabla hujafika nyumbani.
Kusanya nukuu(Quotes)
zote uzipendazo.Nukuu za watu wakubwa ama wabobezi wa jambo fulani ni moja kati
ya vitu muhimu sana vinavyozidisha hamasa(inspiration) kwa mtu mwingine kutenda
jambo kama hilo.Kusanya nukuu uzipendazo zitakusaidia kukupa msukumo wa kufanya
mambo makubwa.
Andika tena historia
ya maisha yako.Uandishi wa historia za maisha yetu ni jambo muhimu sana japo si
wengi wenye utamaduni wa kufanya hivyo,wengi huupuuzia tu na kuona kuwa hamna
haja ya kufanya hivyo,lakini wakiwa hawajui kuwa wanapoteza kitu kikubwa
sana.Unapoandika historia ya maisha yako husaidia kujitathimini kwa siku za
mbeleni kuwa wapi ulipotoka na wapi ulipo sasa,lakini pia kuacha historia yako
siku ukifa ni alama pia.
Piga picha nyingi
kadiri uwezavyo.Katika jambo jingine muhimu sana japo laonekana kama ni la
kawaida kawaida ni hili la upigaji wa picha.Picha zina faida nyingi kwanza ni
kumbukumbuku,lakini pia hukuonyesha taswira halisi ya maisha yako wapi
ulipokuwa na wapi ulipo sasa,siku ukifa watu watazitazama picha zako na
kuendelea kukukumbuka daima,anza leo kupiga picha na uziweke kwenye kumbukumbu
nzuri ikiwa ni kwenye nakala tete(soft copy) au hata kwenye nakala ngumu(hard
kopi).
Wenye hekima wakubwa
walioishi miaka ya zamani walisema; ukitaka kuishi maisha ya kikamilifu fanya
vitu vitatu kabla hujafikwa na umauti,vitu hivyo ni,ZAA MTOTO,PANDA MTI na
ANDIKA KITABU,hivi vitu vitatu si lazima uvifanye vyote japo ukiweza kuvitenda
vyote ni heri.Ukifanikiwa kuwa navyo vitu hivi huwa ni urithi mkubwa utakaokuja
kuuacha duniani,hata siku ukifa lakini hazina hii itaishi kwa miaka mingi sana.
Mwisho kabisa Ishi
maisha ya kikamilifu ili uje kufa ukiwa mtu mwenye furaha.Hapa lipo somo kubwa
sana watu wamekuwa wakiishi mambo ambayo sio kusudio lao waliloitiwa
duniani,unakuta mtu anasoma uhasibu kwa sababu familia yao nzima ni wahasibu
lakini yeye fani hiyo haikiwa wito wake, na hii hupelekea watu kuishi maisha
yenye huzuni na mateso makubwa,inachotakiwa ni mtu uishi kikamilifu katika lile
kusudio lako uliloitiwa hii itakufanya uishi kwa amani na hata siku ukifa utakufa
ukiwa na furaha.
Haya ni machache
niliyotamani nikushirikishe mpenzi msomaji,utakapopata wasaa wa kukisoma kitabu
hiki hakika utajifunza mengi zaidi.Ruhusa kuwashirikisha na wengine tunaoona
wana kiu ya kupata maarifa na kama utakuwa unahitaji kitabu hiki utanipata kwa
barua pepe na namba za simu nitakazo kuachia.Nikutakie heri sana wewe unaenda
kuchukua hatua ya kufanyia kazi.
Na mwanafunzi wa
kudumu wa shule ya maisha, mchambuzi wa vitabu na mshairi;
Marko
Kinyafu
+255
714 129 520
Dar es
salaam,Tanzania.
HAIJALISHI
UMESHAPOTEZA MUDA KWA KIASI GANI,NAFASI YA KUFIKA KULE UNAPOTAKA KUFIKA BADO
IPO KAMA UKIAMUA LEO.