Tafakuri ya
kitabu cha THE POWER OF READING BOOKS(Nguvu ya usomaji vitabu) Na. Shemeji
Melayeki.
Mpendwa rafiki natumai
haujambo,kwa wasaa mwingine natamani nikushirikishe mambo machache ambayo
mwandishi Shemeji Melayaki ameyaelezea katika hiki kifupi kabisa chenye kurasa
14 tu,lakini kikiwa kimesheheni somo kubwa sana,basi nawe karibu twende pamoja.
Watu wakubwa waliowahi
kuwapo na waliopo duniani mafanikio yao ukiwafuatilia utawakuta walikuwa ni
wasomaji wakubwa wa vitabu,tabia ya usomaji vitabu imekuwa ni ngumu sana kwa
watu kuiigia kutokana na uvivu mkubwa watu walionao na hali ya kupenda kuhairisha
mambo na hii hujikuta kuona kama suala la usomaji wa vitabu ni la watu fulani
au la watu wachache lakini hii si kweli,ila mtu yeyote atakae kufanikiwa sharti
asome vitabu ili apate maarifa thabiti katika lile eneo analotaka kujinoa ikiwa
ni katika kipaji,biashara,ujuzi,nk.Tabia huathiriwa na tabia hivyo tabia ya
kutopenda kusoma vitabu itaathiriwa pale tu utakapo chukua uamuzi leo wa kuanza
kusoma vitabu.
Yapo mambo mengi sana mtu hupata faida baada
ya kusoma vitabu,machache miongoni mwa hayo ni kama;
-Maarifa humuongezea
mtu nguvu ya kujiamini na kufanya mambo makubwa kwasababu anakuwa ana uhakika
na lile alifanyalo.
-Maarifa yanamuongezea
mtu nguvu ya ushawishi katika kutekeleza mambo makubwa,kwa sababu vipo vitabu
vingi vinavyolezea jinsi watu walivyofanikiwa katika maisha yao mfano kitabu
cha I CAN,I WILL,I MUST the keys of success kitabu hiki kinaeleza jinsi Dr
Regnald Mengi alivyopitia changamoto nyingi hadi kufikia hapa alipo sasa,hivyo
nawe kupitia kusoma kitabu utapata nguvu ya ushawishi wa kuona kuwa kumbe mambo
makubwa yanawezekana endapo tu ukiamua kweli kuchukua hatua.
-Kitabu huyaunganisha
mawazo ya msomaji na mwandishi wa kitabu kwa kupitia njia ya usomaji.
-Viongozi wote ni
wasomaji vitabu(all leaders are readers),huwezi kuongoza kama hupendi kusoma
vitabu.
-Maarifa ya vitabuni
huunoa ujuzi wako na kukufanya uwe bora zaidi katika eneo lako unalofanyia kazi
ikiwa ni biashara,kipaji,huduma n.k,Mungu mwenyewe hutumia kitabu kuweka
taarifa zake,je si zaidi sana sisi wanadamu? ,Kutoka 32:33
*BWANA akamwambia
Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu
changu.*
MBINU ZA KUANZA KUWA MSOMAJI VITABU.
~Kwanza kabisa tafuta
vitabu vya eneo ambalo unapenda kujifunza hii itakufanya uwe na hamasa ya
kupenda kujifunza kila siku.
~Anza kwa kusoma
kitabu kidogo kwa kuanza na kurasa chache chache mwisho utajikuta ukipiga hatua
siku hadi siku kama vile wenye hekima walivyosema kuwa haba na haba mwisho
hujaza kibaba.
~Soma kila
siku.Usiache tabia ya kusoma japo kwa kurasa chache mwisho utajikuta hii
itakuwa ni tabia yako ya kudumu.
~Fanya tafakuri ya
yale uliyojifunza.Kufanya tafakuri ni sawa na mmeng'enyo wa chakula baada ya
mtu kumaliza kula,nawe ukimaliza kusoma kitabu yaangalie yale uliyojifunza kwa
kupiga picha na jinsi maisha yako halisi yalivyo,kisha chukua hatua ya kutendea
kazi.
~Shirikisha wengine
yale unayojifunza.Usiwe mchoyo wa kuwapa wenzio yale uyajauyo,kwa jinsi
unavyozidi kushirikisha watu kile ukijuacho ndipo unapozidi kuwa bora
zaidi(master) katika eneo hilo.
Anza leo kusoma vitabu
ukianzia kwa hatua ndogondogo huku ukiweka nia ya kutamani kupiga hatua
zaidi.Aonaye kununua kitabu ni gharama kubwa basi asubiri kulipa gharama kubwa
zaidi atayoilipa kwa kutosoma vitabu.Mtu asiyesoma vitabu uhisi dunia ni kama
sehemu ndogo ambayo unaweza kuizunguka na kuimaliza punde kama vile uzungukavyo
kijiji,lakini si kweli,ila uhalisia ni kuwa dunia ina vitu vingi sana ambavyo
kila siku tunatakiwa kujifunza na hatutavimaliza hadi siku tunakufa,basi anza
leo nawe kuishi kiutoshelevu ili uje kufa ukiwa tupu.
Nikutakie heri wewe
uendaye kuchukua hatua katika kutenda na hakika ipo siku utajishuhudia jinsi
utakavyo kuwa mtu mpya siku baada ya siku katika eneo la maarifa.
Mimi Mwanafunzi wa
shule ya maisha,Mchambuzi na mshairi.
Marko Kinyafu.
📩+255 714 129 520
Dar es salaam,
Tanzania.
_Kuyatawala maisha
huanza kwa kuitawala siku moja na siku yenyewe ndio leo_
No comments:
Post a Comment