Tuesday, December 27, 2011

Ndugu Simbakalia Mtumishi aliyetukuka

Imeandikwa na Fadhili Abdallah, Kigoma
Picha kwa niaba ya blogu la bongo ndiyo home
Mkuu wetu wa mkoa wa Mtwara amepatiwa nishani ya Utumishi uliotukuka kwa kanisa na jamii. Hii ni habari njema kwa mkoa wa mtwar. Mchango wake huo ni ule alioutoa kwa taifa hususan kwa mkoa wa kigoma. Kwa Mtwara ni furaha kubwa kwa kuwa tumepata mkuu ambaye ana sifa za uchapaji kazi. Ndugu mkuu wa mkoa endelea na moyo huo ili utakapokamilisha shughuli zako nasi wanaMtwara tutakupatia nishani nyingine bila shaka. Kwa sasa hongera sana kwa mchango wako.










Nishani hiyo ilikabidhiwa kwa Simbakalia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa karibu miaka sita, na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Protas Rugambwa kwa niaba ya Papa katika misa ya Ibada ya Krismasi iliyofanyika kwenye Kanisa la Bikira Maria mshindaji mjini Kigoma.

Simbakalia alitiririkwa na machozi wakati akikabidhiwa nishani hiyo kutokana na kutoamini kile anachokiona hali iliyofanya kanisa kuzizima kwa hali hiyo katika tuzo hiyo ambayo ni ya kwanza kutolewa kwa muumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma tangu kuanzishwa kwake.
Akikabidhi medali na hati ya nishani hiyo, Askofu Rugambwa alisema imetolewa katika kuunga mkono Jubilee ya miaka 50 ya Tanzania Bara ambayo kanisa iliona haina budi kushiriki kwa hali na mali kwa kufanya kitu ambacho kitakumbukwa kwa miaka 50 mingine.

Askofu Rugambwa alisema Simbakalia kama kiongozi wa kijamii, alitumia wakati wake kulitumikia kanisa na kuonesha mchango wake na utumishi wake kwa kanisa bila kujali mamlaka na madaraka aliyonayo.

Akisoma hati hiyo, Katibu wa Kanisa hilo Jimbo la Kigoma, Kiliani Teleba alisema anamtangaza Joseph Simbakalia kutoka Jimbo la Kigoma kuwa shujaa wa ukoo bora wa Mtakatifu Gregory Mkuu wa Daraja la Kiraia na kumpatia uwezo wa kutumia haki zote zinazotokana na hadhi hiyo.

Akishukuru kwa nishani aliyotunukiwa na heshima aliyopewa, Simbakalia alisema wakati akija Kigoma kutumikia nafasi yake ya ukuu wa mkoa, hakuwaza kama siku moja atatunukiwa heshima hiyo kubwa katika kanisa.

Alisema amekaa Kigoma kwa zaidi ya miaka mitano, anaamini amefanya kile alichotumwa kuja kufanya na nishani hiyo ni heshima kwake wananchi wa Mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa jumla kwa heshima waliyopewa ndiyo maana Mungu ameonesha uwezo wake kwa nishani hiyo na heshima aliyopewa.

Naye mke wa Mkuu huyo wa Mkoa, Janet Simbakalia alisema wakati mume wake alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kutoka kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), walijua ni kumkomoa, lakini Mungu ameonesha shani yake kwa yale yote aliyofanya alipokuwa Kigoma.













No comments:

Post a Comment