Tumeambiwa na tunafahamu siku zote kuwa rushwa ni adui wa haki, na ni ya wananchi, ya binadamu, ama ya viumbe vilivyo hai walau kulingana na miongozo na makubaliano yetu. Moja ya makubaliano hayo, kwa Tanzania ni kuwa rushwa ni adui wa haki, na kwenye kanuni/ ahadi za mwana
TANU (chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika) kulikuwa na ahadi ya kutotoa na kutopokea rushwa kwani hupinga ama huzuia watu wengine kupata haki zao.
Katika nchi nyingi duniani, Tanzania ikiwa mojawapo, kuna utaratibu wa kuwa na chombo cha kutolea mawazo, kuihoji serikali iliyo madarakani, kutunga sheria n.k. Chombo hicho kinafanya kazi kwa uwakilishi; si rahisi kwa mwananchi mmoja mmoja kuingia katika chombo hiko kutetea, kudai haki yake ama/ na kufanya shughuli zingine za chombo hicho ambazo kwetu kinajulikana kwa jina la BUNGE. Kwa kuwa si rahisi wote kuingia basi tumelazimika kuwa na wawakilishi wachache ili wawe SAUTI zetu na waseme na kutenda kwa niaba yetu. Hivi karibuni tumesikia habari ya kushangaza juu ya hawa wawakilishi wetu. Tumesoma na kusikia vyombo vya habari vikielezea juu ya baadhi ya wawakilishi wetu hawa wakifanya kile tulichofundishwa kuwa ni adui wa haki, sio lengo la makala hii kuongelea suala hilo bali tu kuiwasilisha makala iliyo katika gazeti la
MTANZANIA inayoeleza juu ya kicha habari.
Mwalimu
JKNyerere aliwahi kusema
IKULU ni patakatifu nadhani
BUGENI halikadhalika ni vivyo hivyo. Je, kama kweli kuna wabunge wameenda kinyume na utakatifu inafaa kweli waendelee kuwepo patakatifu?
Na Arodia Peter .
TUHUMA za rushwa zinazoendelea kuwaandama wabunge, zimechukua sura mpya, baada ya Serikali ya China kujiandaa kupiga marufuku wabunge wote wanaotuhumiwa kujihusisha na rushwa kuingia nchini humo.
Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata kutoka ubalozi wa China hapa nchini, zinasema umepokea taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wakuu wa China, wafuatilie kwa karibu wabunge wote wanaotuhumiwa kwa rushwa, kisha watume taarifa ili wakibainika wasiingie kwenye nchi hiyo.
“Tumeletewa taarifa na viongozi wetu wa ngazi za juu, kuwa tufuatilie kwa kina wabunge wote ambao wanatuhumiwa na wakibainika majina yao yatumwe China, ili wazuiliwe kuingia kule,
…unajua taifa letu ni taifa ambao halina mchezo na mtu anayepokea rushwa ovyo ovyo na ni kosa la jina. kwa kiongozi kama hawa wabunge kujihusisha na siasa,
“Kwa kipindi chote hiki, kama wabunge hawa wangekuwa China leo hii, tungekuwa tunazungumza mambo mengine, wangekuwa wamechukuliwa hatua kali,
“Tunashangaa kuona kwa nini hapa kwenu, bado wanaendelea kuruhusiwa kuingia bungeni… au wanasubiri majibu ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizi,” kilihoji chanzo chetu.
Chanzo hicho, kilisema ubalozi wa China hapa nchini, umetuma maofisa wake mjini Dodoma kwa ajili ya kupata mwenendo wa wabunge wote wanatuhumiwa.
“Hivi sasa hapa Dodoma kuna maofisa wa ubalozi wa China, wanaendesha uchunguzi kuhusu tuhuma hizi, ikibainika ni za kweli baada ya majina ya wabunge ‘wala rushwa’ kutajwa, watachukua picha zao kwa ajili ya kuzituma China, ambako hawataruhusiwa kukanyaga kwa sababu kwao rushwa ni kosa la jinai,” kilisema chanzo chetu.
Naye Mratibu wa maombi yanayoendeshwa na Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania, mjini Dodoma Mchungaji William Mwamalanga alisema kwa kauli moja viongozi wa dini, wamesikitishwa na tuhuma hizo.
Alisema viongozi wa dini ambao wamepiga kambi mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuliombea taifa, wamewataka wabunge wote waliotajwa wajiuzulu mara moja.
“Viongozi wa madhehebu mbalimbali tupo hapa Dodoma, kwa ajili ya kuliombea taifa, lakini moja ya jambo kubwa ambalo tumekubaliana kupita katika majimbo yao, kueleza waumini wetu matatizo haya ya rushwa… tunataka wajiuzulu kwa ajili ya
kulinda heshima zao,