Tamasha la Ngoma za asili la makabila ya mkoa wa Mtwara Maarufu kama Tamasha la MaKuYa limeanza rasmi, huku vikundi mbalimbali vya sanaa vikionyesha umahiri mkubwa katika kucheza ngoma za asili za makabila yao.
Tamasha hilo ambalo mwaka huu lilianza kwa maandamano kutoka katika viwanja vya mashujaa kwenda Uwanja wa Nangwanda maarufu kama uwanja wa Umoja mjini Mtwara limevuta hisia za wakazi wengi wa mji huo na vitongoji vyake ambapo licha kuwepo kwa jua kali, watu waliendelea kumiminika uwanjani, mithiri ya maji mtoni, kushuhudia wasanii wakisakata ngoma mbalimbali.
No comments:
Post a Comment