Hivi karibuni Tanzania ilipewa uenyeji na taasisi ya haki na uzuiaji wa uhalifu ya Afrika Kusini (CJCP), kuendesha mhadhara (kongamano) wa kuzuia uhalifu kwa vijana. Mhadhara huo ilijumuisha wadau wa kada kadhaa: wanawake, vijana, watoto na yote ambayo yanalenga kuzuia uhalifu katika jamii. Mkutano huu ulifanyika hoteli ya White Sands (tarehe 6 - 8 Novemba 2012), Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa kimataifa wa kuzuia uhalifu wa vijana katika jamii White Sands Dsm 6-8 Nov 2012 |
Mhadhara huu ulikuwa na mada anuwai zilizofanyiwa kazi. Malezi mema kwa watoto wangali wadogo kabisa, Njia mbadala za kuzuia uhalifu katika jamii, Polisi jamaa na vijana, Njia mbadala na fursa za kazi kwa vijana na kadhalika.
Ndugu Mandalu akitoa mada juu ya njia mbadala kupunguza uhalifu miongoni mwa vijana |
Wanamhadhara walitoka zaidi ya nchi ishirini na tano za mabara karibu yote ya dunia. Kwa hakika ilikuwa ni fursa nzuri kusikia wadau wa haki na amani wanavyofanya kazi kufanya dunia kuwa sehemu njema na ya kufaa kuishi sisi sote. Wanataaluma hawakuachwa kando pia, waliwasilisha tafiti zao zenye kutoa maelekezo na mwongozo wa namna ya kupunguza uhalifu katika jamii, wakati huo huo vijana, ambao ni wahanga wa fujo na wanawezeshwa kuondokana na adha hiyo. Inafahamika vyema kuwa wadau wakuu wa ujenzi wa dunia ni vijana, kwa kuwa ni kundi la watu wenye uwezo na nguvu kazi kubwa; kwahiyo basi ni muhimu kuwalea vyema wadau hao.
Ndugu Muchunguzi akiwasilisha mada juu ya malezi |
No comments:
Post a Comment