Nchi ya Tanzania, inaendelea na mchakato wake wa kuandika katiba mpya yenye mguso wa moja kwa moja toka kwa WaTanzania walio wengi. Katika juhudi hizo wadau mabalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi, watu binafsi na kadhalika wanafanya juhudi kuwaelimisha wananchi walio wengi na wasio na ujuzi na uelewa wa katiba inayotumika nchini hivi sasa. STEMMUCO kwa nafasi yake imefanya kazi hiyo ya kuwaelimisha wanachuo juu ya katiba inayoiongoza Tanzania kwa sasa. Idara ya sheria, chuoni hapo imeongoza mhadhara wa wazi kwa wote waliopenda ili kuielezea katiba hiyo.
No comments:
Post a Comment