Thursday, September 27, 2012

SIKU YA UTALII TANZANIA NA DUNIANI

Kazi ya Sanaa Mji mkongwe MIKINDANI
Wanayama wakivuka mto huko Serengeti - Tanzania



Sanaa MIKINDANI - MTWARA

Faru weusi huko Ngorongoro - Tanzania





















Leo ni siku ya UTALII TANZANIA NA DUNIANI: Utalii ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya uchumi duniani. Kuna nchi kadhaa ambazo hutegemea tu uchumi kujiendesha na kuendelea kuwepo. Kikubwa ni uwekezaji wa makusudi na lazima katika sekta hiyo yenye uwezo wa kuzalisha ajira lukuki. Tanzania ina mali asili nyingi mno ambazo ni vivutio tosha vya utalii; moja ya mambo yanayoturudisha nyuma katika hili ni uwekezaji hafifu kwa watu wetu.

 Uwekezaji huu utazame kwa makini hasa aina ya elimu tuitoayo kwa wanafunzi wetu; kwa kuwa tuna vivutio vingi vya utalii basi tuwe na mitaala yenye kulenga utalii toka shule ya msingi. Shule zetu ziwe na michepuo yenye kuendana na mahitaji ya karne ya ishirini na moja. Kuwe na shule zenye kuangazia masomo ya sayansi na teknolojia yenye kujibu mahitaji ya moja kwa moja ya watu wetu. Tukirudi kwenye utaliii, shule na mitaala yenye kufunza huo utalii zianze mapema kufunza yaliyo ya lazima; uaminifu, ukarimu, lugha za kigeni, na mengine muhimu hiyo itasaidia kutumia vyema rasilimali na utajiri mkubwa tuliopatiwa na Mwenyezi Mungu, kinyume na hivyo tutaendelea kuwalaumu majirani waliojipanga kunufaisha jamii zao na hiyo nd'o hasa jukumu la serikali.    


No comments:

Post a Comment