Tuesday, September 13, 2011

Vijana na Mabadiliko

Makala ya Mwandishi Ahmed Rajab; Vijana wa Afrika wanawaperemba tu viongozi... imejaa mambo anuai ambayo yana manufaa mengi kwa kijana mwenye malengo ya kuchangia katika jamii yake.

Mwandishi anaongelea mwamko mpya wa vijana barani Afrika katika kudai haki za jamii zao, aidha anatoa picha ya jinsi viongozi wabadhilifu wanavyo tumia vibaya mali za umma kwa manufaa binafsi.

Jambo jingine ambalo najifunza hapa ni juu ya watoto wa viongozi wabadhilifu wanavyorithi tabia na hulka za wazazi wao. Pengine hili ni jambo jema kwa watoto wa viongozi kufanya uchunguzi wa maisha yao binafsi. Mwanafalsafa Socrates anatualika binadamu kufanya tafakari ya nafsi zetu. Maisha ambayo hatuyafanyii tafakari hayafai kuyaishi. Hivyo watoto wa viongozi hususani viongozi badhilifu wanaweza kuishi maisha yao binafsi bila kufuata mfano mbaya wa maisha ya wazazi wao.

Suala jingine kwa mwandishi Ahmed Rajab, ni utaalamu wake wa lugha, kupitia makala zake unaweza kuiweka sawa lugha yako ya Kiswahili; binafsi naona ni mtaalam wa ngazi ya juu kabisa ya Kiswahili.
Asante kwa makala nzuri toka barazani kwako!

No comments:

Post a Comment