Wanachuo wakifanya mitihani yao Picha kwa Hisani ya wadau wa blogu |
Tunawatakia mafanikio katika mitihani yao. Mitihani kwa maoni yangu si kipimo bora zaidi kuliko vipimo vingine, ila ndo kipimo cha uelewa kinachokubalika, inawezekana kabisa kukawa na njia nyingine bora zaidi lakini bora hazijakubalika.
Kwa kuwa mitihani ndo njia inayokubalika kupima uwezo wetu basi tuiheshimu na kuifanya kwa bidii na maarifa. Bidii na maarifa vinatakiwa kuja wakati wa maandalizi ili kuweza kumudu na kutawala somo kabla ya kuingia chumba cha mitihani. Ni m uhimu kufanya hivyo ili kujiamini katika kufanya mitihani, kuthibitisha utu na maadili yetu. Ni vyema mtu akafanya mitihani yeye mwenyewe bila kutumia vyanzo visivyoruhusiwa. Kufanya hivyo ni kipimo cha utu bora na faida kwa taifa na dunia kwa ujumla, kwani viongozi na watu wema wamo miongoni mwa wanavyuo wanaoendelea na mitihani yao hivi sasa.
Ili kujijenga zaidi kitaaluma nhapa chini kuna nafasi ya masomo ya uzamili kwa wanaopenda ila nafasi ijazwe haraka kwa kuwa muda umekwisha. Fanya haraka kupata nafasi hii:
MASTERS STUDIES - MPhil in African Studies
Our aim is to offer students a window into the cultural, intellectual, and political dynamism of African societies. At a time when Africa is often represented a place in need of outsiders' benevolence and direction, we hope to give students the linguistic and interpretive tools to study African societies on their own terms. The degree will provide an excellent foundation for those who wish to expand their knowledge of Africa, and particularly for students entering positions in the arts, the media, NGOs, and other professions.
The application deadline for MPhil in African Studies 2012-13 is the 30 June 2012
KWA TAARIFA ZAIDI SOMA HAPA