Saturday, January 30, 2016
ORODHA YA VYUO VIKUU BORA TANZANIA 2015
ORODHA YA VYUO BORA NIGERIA 2015
VYUO BORA NCHINI NIGERIA
1 University of Lagos Lagos
2 Obafemi Awolowo University Ile-Ife
3 University of Ibadan Ibadan
4 University of Ilorin Ilorin
5 Covenant University Ota
6 Federal University of Technology, Minna Minna
7 University of Nigeria Nsukka
8 University of Benin Ugbowo
9 University of Port Harcourt Port Harcourt
10 Ahmadu Bello University Zaria
11 University of Agriculture, Abeokuta
12 Landmark University Omu-Aran
13 Rivers State University of Science and Technology Port Harcourt
14 Federal University of Technology, Akur, Akure
15 University of Jos Jos
16 Nnamdi Azikiwe University Awka
17 Lagos State University Ojo
18 Redeemer’s University Mowe
19 Bayero University Kano Kano
20 University of Maiduguri Maiduguri
21 Ladoke Akintola University Of Technology Ogbomoso
22 Federal University, Dutsin-Ma Dutsin-Ma
23 Federal University of Technology, Owerri Owerri
24 Federal University, Oye-Ekiti Oye
25 Afe Babalola University Ado-Ekiti
26 Osun State University Oshogbo
27 Paul University Awka
28 Ekiti State University, Ado Ekiti Ado-Ekiti
29 Adekunle Ajasin University Akungba Akoko
30 Federal University, Dutse Dutse
31 University of Uyo Uyo
32 University of Agriculture, Makurdi, Makurdi
33 University of Abuja, Abuja
34 Ebonyi State University Abakaliki
35 Veritas University Abuja
36 Madonna University Okija
37 University of Calabar Calabar
38 Nasarawa State University Keffi
39 Pan African University Lagos
40 Ambrose Alli University Ekpoma
41 Lead City University Ibadan
42 Abubakar Tafawa Balewa University Bauchi
43 Kwara State University Ilorin
44 Delta State University, AbrakaAbraka
45 Baze University Abuja
46 Bingham University Auta Balifi
47 Bells University of Technology Ota
48 Umaru Musa Yar’Adua University Katsina
49 Babcock University Ilishan-Remo
50 Federal University of Petroleum Resources Effurun
51 Benue State University Makurdi
52 Enugu State University of Science and Technology Enugu
53 Joseph Ayo Babalola University Ikeji-Arakeji
54 Niger Delta University Wilberforce Island Yenagoa
55 African University of Science and Technology Abuja
56 Kaduna State University Kaduna
57 Federal University, Lokoja Lokoja
58 Igbinedion University Okada Okada
59 Ibrahim Badamasi Babangida University Lapai
60 Fountain University Oshogbo
61 American University of Nigeria Yola
62 Achievers University, Owo Owo
63 Ondo State University of Science & Technology Okitipupa
64 Obong University Obong Ntak
65 Crawford University Faith City
66 Federal University, Otuoke Otuoke
67 Anambra State University Uli
68 Olabisi Onabanjo University Ago Iwoye
69 Tai Solarin University Of Education Ijebu-Ode
70 Modibbo Adama University Of Technology Yola
71 Ajayi Crowther University Oyo Town
72 Imo State University Owerri
73 Caleb University Imota
74 Federal University, Ndufu-Alike Ndufu-Alike
75 University of Mkar Mkar
76 Nigerian Turkish Nile University Abuja
77 Novena University Ogume
78 Adeleke University Ede
79 Renaissance University Enugu
80 Al-Hikmah University Ilorin
81 Caritas University Enugu
82 Usmanu Danfodio University Sokoto
83 Kebbi State University Of Science and Technology Aliero
84 Benson Idahosa University Benin City
85 Oduduwa University Ile Ife
86 Michael Okpara University Of Agriculture Umuahia
87 Bowen University Iwo
88 Adamawa State University Mubi
89 Crescent University Abeokuta
90 Cross River University Of Science & Technology Calabar
91 Gombe State University Gombe
92 Elizade University Ilara-Mokin
93 Abia State University Uturu
94 Wellspring University Benin City
95 Yobe State University Damaturu
96 Western Delta University Oghara
97 Federal University, Lafia Lafia
98 Wesley University Of Science and Technology Ondo City
99 Bauchi State University Gadau
100 Federal University, Kashere Kashere
101 Federal University, Wukari Wukari
102 Samuel Adegboyega University Ogwa
103 Taraba State University Jalingo
104 Sokoto State University Sokoto
105 Kwararafa University Wukari Wukari
106 Tansian University Umunya
107 Akwa Ibom State University Uyo
108 Godfrey Okoye University Ugwuomu-Nike
109 Salem University Lokoja
110 Plateau State University Bokkos
111 Katsina University Katsina
112 Kogi State University Anyigba
113 Rhema University Aba
http://nigerianuniversityscholarships.com/list-best-universities-nigeria-2015-nuc-share/
Friday, January 29, 2016
JE AFRIKA TUNAWEZA KUMUDU ELIMU BORA NA BURE?
JE, AFRIKA INAWEZA KUMUDU ELIMU BURE?
Mjadala umeendelea kote barani Afrika kupitia mtandao wa Bbc. Swali hili ni muhimu kwa Tanzania pia. Je, tunaweza kumudu elimu bure? Elimu hiyo ya bure inafaa iendane na ubora pia si tu elimu bure lakini yenye ubora bure pia.
Kwenye picha iliyochukuliwa mtandao wa bbc wanaonekana watoto wakiwa kwenye darasa la chini ya mti, wakiwa wamekalia mawe ili hali wapita njia wakiendelea na shughuli zao. Ama kwa hakika hapa ni ngumu mno kupata elimu bora hata kama itakuwa bure...
http://www.bbc.co.uk/programmes/p03g5pbx
Wednesday, January 20, 2016
SABABU ZA UGUMU WA MAISHA MTWARA ZATAJWA...
Mkoa wa Mtwara ni moja kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Mkoa huu una sifa lukuki moja ya sifa hizo ni ugumu wa maisha; mkoa huu unasifika kwa bei kubwa za bidhaa ikilinganishwa na mikoa mingine ya nchi. Kwenye moja ya vipindi vyake maarufu vya jioni kituo cha redio PRIDE FM kilichopo mkoani humo siku ya Jumanne tarehe 19 Januari 2016 iliendesha kipindi ambacho pamoja na mambo mengine kilihoji kwanini maisha bidhaa mbalimbali katika mkoa huo ukilinganisha na mikoa mingine ni aghali zaidi?
Washiriki waliopiga simu walikuwa na majibu anuwai; mmoja kati ya wapiga simu hao alisema ni kweli kwamba maisha ni magumu Mtwara ikilinganishwa na mikoa mingine na sababu hasa ni uvivu wa wakazi wa mkoani humo. Wakazi wengi wanaojishughulisha na kilimo hulima eneo dogo tu la shamba na kutaka kuendesha maisha yao kupitia shamba hilo. Jambo hilo huwalazimu wakulima hao kupanga bei kubwa za mazao yao pindi wakati wa kupeleka bidhaa sokoni unapofika.
Mchangia mada mwingine alisema sababu hasa ni zile za kihistoria kwamba bidhaa zilizotoka mikoa ya jirani zilipangiwa bei kubwa kwa kuwa barabara kwenda mkoani humo zilikuwa mbovu mno na hivyo kufanya gharama za usafirishaji kuwa kubwa jambo liliongeza bei ya bidhaa.
Wito umetolewa kwa serikali kulitazama upya suala la bei za bidhaa mkoani humo kwa kuwa barabara imejengwa kwa kiwango cha lami na hivyo hakuna tena sababu ya gharama kubwa za usafirishaji.
Sunday, January 17, 2016
JIMBO KATOLIKI MTWARA LAPATA ASKOFU
Titus Joseph Mdoe, amesimikwa rasmi hivi leo kuwa askofu wa tano wa jimbo katoliki Mtwara. Askofu Mdoe aliteuliwa mwaka 2015 na Papa Fransisko kuliongoza jimbo hilo kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa askofu wa jimbo hilo Gabriel Mmole. Askofu Mmole ambaye amelitumikia jimbo la Mtwara kwa miaka 31 anastaafu kisheria kwa mujibu wa kanuni za kanisa.
Askofu Mdoe amesimikwa rasmi mbele ya umati mkuu wa maaskofu toka pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa ngazi mbalimbali za serikali na halaiki kuu ya waumini na watu wenye mapenzi mema mkoani Mtwara.
Wednesday, January 13, 2016
MBORESHA DUNIA KWA NYIMBO ZA DINI
EVA STESHENI MWIMBA NYIMBO ZA DINI |
Tuesday, January 12, 2016
MAPINDUZI DAIMA
Picha na mtandao |
Leo 12 Januari 2016 ni kumbukumbu ya 52 ya siku ya mapinduzi yaliyofanyika visiwani Zanzibar mwaka 1964. Mapinduzi hayo yalifanyika ili kufanikisha utawala wa wengi dhidi ya utawala wa wachache. Mapinduzi hayo yalifanyika kuuong'oa utawala wa Sultan wa kiArabu aliyekuwa amepata uhuru toka mikononi mwa Waingereza. Waarabu walikuwa wachache lakini wakapewa mamlaka na Waingereza, Wazinzibar wenyeji na wenye asili ya Afrika wakafanya mapinduzi hayo kuchukua haki yao.
Mapinduzi Daima ndiyo hasa salaam rasmi kwa siku hii na hii inakubaliana na maneno ya Heraclitus mwanafalsafa wa kale wa Kigiriki aliyekuwa wa mwanzo kusema hakuna kinachodumu ila mabadiliko, ama mapinduzi hivyo ni hakika na sahihi kusema mapinduzi daima.
Tunawapongeza wananchi wote waZanzibar na Tanzania kwa ujumla wao. Aidha maadhimisho haya yawe ni chachu ya kutanzua mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani humo ili nchi indelee kuwa ya amani na salama.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake...
Thursday, January 7, 2016
DHANA YA KUTUMBUA MAJIPU IMETOKA WAPI?
Picha kwa hisani ya mtandao |
Wakati wengi wetu
tukiendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu JPMagufuli
kwa kushughulikia vilivyo matatizo yanayoisibu nchi, wachache tu kati yetu
tumejiuliza kwanini kaamua kutumia dhana hiyo aliyoichagua kutatua matatizo
yanayoikumba nchi Dr JPM ameamua kutumia dhana ya kutumbua majipu kama
kiwakilishi cha utatuzi wa matatizo mazito, sugu na yaliyo kero kubwa kwa
wananchi wa Tanzania. Wengi wetu tuliisikia kauli na dhana hiyo siku alipoongea
na wabunge wa bunge wa la Jamhuri ya Muungano siku ya uzinduzi wa bunge.
Kupata jibu kwanini
aliamua kutumia dhana hiyo, kuna njia kuu mbili; ya kwanza ni kumuuliza yeye
mwenyewe ndugu JPM na ya pili ni kuutumikisha ubongo kufanya shughuli hiyo.
Njia ya kwanza japokuwa ni fupi, nyepesi na inatoa jibu sahihi, si njia
tunayoitamani. Hatuitaki njia hiyo kwakuwa haijengi uwezo wa kufikiria kwa
namna sahihi. Ila hali njia ya pili ni ndefu, inashughulisha, inaimarisha uwezo
wa ubongo, inakomaza uwezo wa ubunifu na kadhalika. Zaidi njia hii ya pili
inachosha lakini hasa ndiyo tunapaswa kuifuata kwa kuwa inazalisha faida nyingi
zaidi mbali ya jibu ambalo huenda lisiwe sahihi licha ya kutumia muda mrefu
kulipata. Hiyo ndiyo hasa kazi ya falsafa; kujenga uwezo kuuliza maswali sahihi
na kupitia njia sahihi za tafakari kujenga fikra sahihi ili hali ikiwa ni
kutafuta UKWELI.
Tukirejea kwenye swali
letu la msingi je kwanini JPM ametumia dhana ya kutumbua majipu? Ama ametoa
wapi dhana hii? Katika falsafa na jinsi ninavyoamini pia kila kitu tumekipata
maishani, ama tumekiishi sisi wenyewe, ama tumeona kwa wengine, ama tumesikia,
ama kuhisi toka kwa wengine, ama kwa ufupisho huyapata mambo haya kupitia
milango yetu ya fahamu za hisia (kuona, kusikia, kunusa, kuhisi na kuonja) haya
ndiyo mafundisho ya wanafalsafa kadhaa wakiongozwa na Aristotle. Kwa upande wa
wale wanaoongozwa na Plato; mwalimu wa Aristotle na mwanafunzi wa Socrates, wao
wanaamini kuwa tuliishi sehemu nyingine kabla ya kuja hapa duniani na hivyo
tulifahamu mambo yote huko tulikoishi. Hivyo mambo yote tunayofanya hivi sasa
ikiwa ni pamoja na elimu ni juhudi tu za kujikumbusha tuliyoyaishi hapo kabla
katika ukamilifu wa maisha. Unaweza kutumia mtazamo wowote kati ya hii miwili
kupata jibu. Kwa Makala hii/haya twatumia mtazamo wa kiAristotle kupata jibu na
hivyo ndugu JPM katumia dhana ya kutumbua majipu toka kwenye Hasina ya
kumbukumbuu zake.
google image |
Kwahiyo basi dhana ya
kutumbua majipu ndugu JPM ama ameiishi yeye mwenyewe, ama kaishuhudia kwa mtu
mwingine, ama alipata kusimuliwa juu ya dhana hiyo na mtu mwingine. Pengine
kabla ya kuendelea tujiulize kwanza jipu ni nini? Kwa mujibu wa Kamusi ya
Kiswahili Sanifu ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar es Salaam (TUKI),
jipu ni uvimbe mkubwa unaotunga usaha. Na usaha ni ute wa rangi y manjano
iliyopauka unaotunga aghalbu katika vidonda na majipu. Kamusi hii inaeleza tu
maana ya jjipu na usaha. Lakini katika uhalisia wa maisha jipu ni adha inayousumbua
mwili na kuufanya ufanye kazi zake kwa taabu. Zaidi uvimbe huu mara nyingi,
bila shaka kuna sababu za kitabibu, huvimba maeneo yenye kumkosesha Amani na
kumpatia binadamu usumbufu uliokithiri. Unaweza kukuta jipu limempata mtu
kwenye makalio, mgongoni, sehemu zake za siri na kadhalika. Fikiria mtu mwenye
kazi ya inayomlazimu kuketi muda mwingi, apatwe na jipu kwenye makalio…bila
shaka unapata picha ya adha kubwa ndugu huyo atakayoipata.
Mtu huyo anahitaji
matibabu ya haraka ili aendelee na kazi zake ili kutumia vipawa vyake, kuitegemeza familia, jamaa zake, na taifa
lake, kinyume na hapo familia jipu litamhangaisha na familia yake itaathirika,
nchi itakosa mchango wake wa kimaendeleo. Kuepuka yote hayo mgonjwa anakwena
hospitali kutumbuliwa jipu hilo. Kutumbua jipu hilo ni moja ya njia za kutibu uvimbe
huo, nyingine inaweza kuwa vidonge vya kupunguza uvimbe na hatimaye kuisha.
Kati ya njia hizi mbili, madaktari wanaweza kutujuza kama zipo njia nyinge
murua zaidi yaa hizi mbili, ile ya kutumbua jipu ni bora zaidi kwa kuwa njia
hii huasaidia kuondoa pia kiini cha jipu na hivyo kuzuia jipu hilo kuhamia
sehemu nyingine ya mwili.
Hivyo basi utaona kuwa
dhana ya Rais Magufuli ya kutumbua majipu imejengwa toka katika uhalisisa wa
maisha yanayofahamika kwa watu wengi. Hivyo umithirishaji wa matatizo yanayoikumba
jamii ya watanzania na tatizo la majipu mwilini ni dhana inayoeleweka kwa
urahishi na hivyo inaweza kuimarisha na kuhamasisha uungwaji mkono na ushiriki
wa watanzania wengi zaidi katika jitihada za kutumbua majipu (juhudi za kutatua
matatizo yanayowaumiza wananchi na kubana fursa zao za kujiletea maendeleo).
Kwa hiyo basi ndugu JPMagufuli huenda akawa anatumia dhana hiyo kwa kuwa
anafahamu kero za majipu mwilini na jinsi ambavyo huwa kero kubwa na kubana
fursa za mhanga kufanya shughuli zake za kila siku.
Mandalu
Monday, December 28, 2015
MAISHA NI MALENGO
Leo ni mwanzo wa juma jipya, mwezi mpya, mwanzo wa miezi mipya kumi na mbili ama maarufu zaidi mwaka mpya.
Mwanzoni mwa mwaka ni kipindi kizuri kufanya tathmini ya kile tulichokuwa tukikifanya kama hatukufanya hivyo mwishoni mwa mwaka. Ama yaweza kuwa fursa ya kuweka malengo mapya ama kuyapitia yaliyotangulia kwaajili ya muda mpya unaoanza mbele yetu.
Kufanya tathmini ama kujiwekea malengo katika maisha ni suala la msingi mno kama tunataka kuishi katika namna inayoeleweka na yenye tija na mchango katika dunia yetu. Lengo la maisha kwa kila binadamu awe anafahamu ama la ni kuwa na furaha maishani. Aristotle, mwanafalsafa wa kale anasema hivyo pia; ili mtu awe na furaha basi hana budi kujiwekea malengo. Malengo huwekwa na watu wa kila kada.
Mwalimu shuleni hujiwekea malengo yake, mwanafunzi, mwanasiasa, mwanamichezo, mwanasanaa, mwanauchumi, msomi, mwanazuoni, mwanasheria, mkufunzi, mfanyabiashara, mkulima, mchungaji kanisani, shehe msikitini, imamu sinagogini, na kadhalika…watu wote makini wa kada zote hujiwekea malengo maishani. Kutokuwa na malengo maishani ni mithili ya muuza duka bila daftari, ambapo twajua mali bila daftari hupotea bila habari. Maisha bila malengo hupotea bila taarifa.
Kujiwekea malengo ni utamaduni ambao inafaa watu wote tuwe nao. Kwa kusema hivyo nafahamu fika kuwa kuna ndugu wasio na mazoea ya kufanya hivyo; watu hao mara nyingine hufananishwa na bendera fuata upepo hufuata chochote kitakachokuwa mbele yao. Bila ubishi si utaratibu mzuri wa maisha. Kwa wasio na utaratibu huo ni wakati sawia kuuanzisha.
Dini nyingi hutueleza kuwa hapa duniani ni sehemu tu ya mpito - twapita tu na kwamba makao yetu halisi yapo kwa muumba wetu. Hivyo wakati tukiandika malengo yetu ya maisha ni vyema tukamshirikisha huyo muumbaji kwa kuwa sisi hatujui siku wala saa ya kuyahama makazi ya hapa duniani, japokuwa hatutakiwi kuogopa kifo.
Unapoandaa malengo fanya hivi:
Kwa wanandoa, ama watarajiwa, wawashirikishe wenzi wao. Malengo haya si yako peke yako. Kwa hiyo nafsi ya kwanza ni Mwenyezi Mungu na pili ni mwenzi wako wa maisha; mkeo, mumeo ama mchumba wako. Muombe(ni) Mungu ili awaangazie kufanya malengo ya kweli.
Hatua ya pili ni kuwa mkweli na hali yako halisi; weka malengo ambayo yana uhalisia wa maisha yako. Mfano haina maana kwako mwanafunzi wa Tanzania kuwa na lengo la kuwa rais wa Pakstani miaka mitano ijayo. Weka malengo ambayo kwa kiasi fulani una nafasi ya kuyatekeleza. Mfano kusoma kozi ya Kifaransa kwa undani mara baada ya kumaliza masomo yako mwezi wa Juni.
Weka malengo yenye kukujenga na yatakayohitaji juhudi zako kuyatimiza.
Usiogope kuwa na malengo mengi bora tu ni muhimu katika makuzi na utu wako, mwisho wa muda wa kuyatimiza utakapowadia utakuwa na wasaa wa kujitathmini na kujua wapi ulihitaji ama utahitaji juhudi zaidi. Mara nyingine tukiwa na malengo mengi na yenye kudai juhudi zetu zaidi ndipo ambapo huwa na mafanikio zaidi maishani.
Usiwe mtu wa kujihurumia; kuona kuwa malengo haya ni mengi na magumu mno siwezi kuyatimiza. Usishindwe kujaribu, jaribu kutenda na ukishindwa wakati ukitenda ni tofauti kabisa na ukishindwa kujaribu kufanya chochote.
Jiamini na usijilaumu. Fanya utakachoweza kwa juhudi zako na mambo yakienda kombo, bila shaka utapata fursa nyingine ya kutenda tena!
Kila la heri na Mungu akubariki!
Mandalu
01/01/2012
Mandalu
01/01/2012
Tuesday, December 15, 2015
MAGUFULI APASUA VICHWA WASOMI
WAKATI wananchi wengi wakipongeza hatua ya Rais Dk. John Magufuli kuelekeza pesa zilizochangwa kwa hafla ya kuzindua Bunge kununua vitanda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wapinzani wake wanaeleza huo ni mwanzo wa kushindwa katika vita dhidi ya ufisadi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Profesa Mwesiga Baregu amesema hatua ya Rais Magufuli kupokea pesa hizo bila kuhoji malengo na msingi wa Mhimili huo wa kutunga sheria kuchangiwa fedha ni ishara ya wazi kuwa ameingia kwenye mtego wa ufisadi wa kimfumo.
“Bunge ni taasisi nyeti sana kuruhusu kuchagiwa pesa na watu ambao linapaswa kuwasimamia, hizi taasisi za fedha zilizochangia zinaweza kujikuta zinatakiwa kuchunguzwa na Bunge, credibility yake itakuwa wapi. Angeuliza kwanza kwanini wamechangisha pesa hizo, nani anawajibika nazo?
“Kama anasimamia uadilifu hakupaswa kuchukua tu hela ambazo zimechangwa bila kujua dhamira za wachangiaji, huko tunakokwenda tunahitaji miswada ya kusimamia sekta ya fedha, sheria za kodi wanapolipia dhifa ya kwanza ya kufungua Bunge, huu ni mtego, kwani Bunge haliwezi kupewa uwezo wa kuchukua hazina kiasi kidogo hata kama ni shilingi milioni tano kufanya mambo yake, dignity (heshima) yetu iko wapi kama tuna Bunge omba omba na hatujui dhamira za wachangiaji?” alihoji Profesa Baregu.
Aliongeza kwamba huo ndiyo ufisadi wa kimfumo unaoitesa Tanzania, huku akiweka wazi kuwa anazofanya sasa Rais ni mbio za sakafuni kwa kuwa hawezi akadumu na hali hiyo.
“Mkapa (Benjamin, Rais wa awamu ya tatu) alianza na kasi kuliko hata hii, pamoja na juhudi kubwa za Mwalimu Nyerere, kumtangaza kuwa Mr. Clean, kuunda Tume ya Warioba kuhusu rushwa na kuwa na baraza aliloiita la askari wa miavuli, ameishia wapi, katika kipindi chake ndiyo kashfa nyingi za ufisadi zimeibuka. Simuoni kama atakuwa tofauti na watangulizi wake,” alisema.
Ni kama Nyerere
Wakati Profesa Baregu anayatazama mambo kwa jicho hilo mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Dk. Charles Kitima ameliambia Raia Mwema kuwa Rais Magufuli, amejipambanua kuwa ni aina ya kiongozi anayeweza kutekeleza anayoyasema kutokana na rekodi yake ya utendaji.
Amemweleza Rais Magufuli kuwa ni kiongozi wa kipekee ambaye hotuba yake ya kuzindua Bunge imeonyesha ni jinsi gani anaweza kuunganika na wananchi masikini wa ngazi ya chini.
“Hotuba yake imegusa watu wa kawaida kabisa, kama zilivyokuwa hotuba za Mwalimu Nyerere, anasema kwa lugha inayotoka moyoni, pengine ni kwa sababu ameishi maisha ya kawaida, ndiyo maana ameweza kuwavutia wengi,” alisema Dk. Kitima.
Aliongeza kwamba ingawa hotuba za mwanzo za viongozi ni kujaribu kuwaaminisha wananchi kwamba atatekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni, utekelezaji wa ahadi hizo hutegemea aina ya kiongozi husika.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge pamoja na mambo mengine aliwekea umuhimu suala la kubana matumizi ya serikali ili fedha zinazookolewa zielekezwe kwenye huduma za jamii.
Ili kuonyesha alivyodhamiria kulitekeleza hilo, juzi Jumatatu, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema Rais Magufuli ameagiza kufutwa kwa sherehe za uhuru ili watu watumie siku hiyo kufanya kazi ya usafi.
“Hatuwezi kusherehekea miaka 54 ya Uhuru huku tukiendelea kusumbuliwa na ugonjwa wa kipindupindu unaoweza kuzuilika kwa kufanya usafi tu. Hii ni kejeli kwa taifa huru kwa zaidi ya miaka 50.
“Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wameagizwa kununua vifaa vya kufanyia usafi ili siku hiyo tuiadhimishe kwa utaratibu maalumu wa kupambana na kipindupindu,” alisema Balozi Sefue.
Akizunngumzia hotuba hiyo, aliyekuwa mtia nia ya kuwania urais kupitia CCM, Williamu Ngereja alisema hotuba hiyo ya Rais Magufuli ni mwanzo mpya kwa taifa.
“Hotuba ya Rais Magufuli ni mwongozo sahihi kwa taifa letu kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Kama wananchi wanataka mabadiliko ya kweli, kama walivyoonyesha kwenye kampeni, kila mtu anapaswa kumuunga mkono,” alisema Ngeleja. -
CHANZO CHA HABARI HII :http://www.raiamwema.co.tz/magufuli-apasua-vichwa-wasomi
Subscribe to:
Posts (Atom)