Mkoa wa Mtwara ni moja kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Mkoa huu una sifa lukuki moja ya sifa hizo ni ugumu wa maisha; mkoa huu unasifika kwa bei kubwa za bidhaa ikilinganishwa na mikoa mingine ya nchi. Kwenye moja ya vipindi vyake maarufu vya jioni kituo cha redio PRIDE FM kilichopo mkoani humo siku ya Jumanne tarehe 19 Januari 2016 iliendesha kipindi ambacho pamoja na mambo mengine kilihoji kwanini maisha bidhaa mbalimbali katika mkoa huo ukilinganisha na mikoa mingine ni aghali zaidi?
Washiriki waliopiga simu walikuwa na majibu anuwai; mmoja kati ya wapiga simu hao alisema ni kweli kwamba maisha ni magumu Mtwara ikilinganishwa na mikoa mingine na sababu hasa ni uvivu wa wakazi wa mkoani humo. Wakazi wengi wanaojishughulisha na kilimo hulima eneo dogo tu la shamba na kutaka kuendesha maisha yao kupitia shamba hilo. Jambo hilo huwalazimu wakulima hao kupanga bei kubwa za mazao yao pindi wakati wa kupeleka bidhaa sokoni unapofika.
Mchangia mada mwingine alisema sababu hasa ni zile za kihistoria kwamba bidhaa zilizotoka mikoa ya jirani zilipangiwa bei kubwa kwa kuwa barabara kwenda mkoani humo zilikuwa mbovu mno na hivyo kufanya gharama za usafirishaji kuwa kubwa jambo liliongeza bei ya bidhaa.
Wito umetolewa kwa serikali kulitazama upya suala la bei za bidhaa mkoani humo kwa kuwa barabara imejengwa kwa kiwango cha lami na hivyo hakuna tena sababu ya gharama kubwa za usafirishaji.
No comments:
Post a Comment