Monday, November 23, 2015

FURSA KWA VIJANA KUSAFIRI NA KUJIFUNZA NCHINI AFRIKA KUSINI



Warsha kwa vijana wa kati ya miaka 18 - 25 itafanyika huko nchini Afrika Kusini mwezi September 2016. Ili kushiriki kijana anatakiwa kujaza fomu ya maombi mtandaoni mapema na mwisho ni tarehe 4 Desemba 2015


Calling Young Leaders in Conservation and Animal Protection: Ages 18-25

In September 2016, the first Youth Forum for People and Wildlife will take place in Johannesburg, South Africa. Twenty young leaders working in animal and conservation-related fields from around the world will connect with experts, explore solutions, and build skills that will help them better understand wildlife conservation issues from multiple perspectives and empower them to become compassionate conservationists. Travel and participation costs covered.

Friday, November 20, 2015

WANASIASA KAMA WANANDOA!!!

Image by google
Makundi haya mawili yote hula kiapo cha utii na uaminifu mbele za watu na Mungu lakini bado wanachakachua!!!

WANANDOA:
Image by google

Watu wawili kwa kawaida mtu mme na mtu mke wanapopendana na kukubaliana kuishi pamoja hulazimika kuweka wazi suala hilo mbele ya umma wa wanajamii wanaoishi nao. Kwa kawaida watu hawa hula kiapo, huwekeana ahadi kuwa watakuwa waaminifu baina yao na kawaida huomba msaada wa Mungu awawezeshe kuwa waaminifu katika kiapo chao. Hufanya hivyo na kuahidi kuwa wavumilifu katika jua na mvua, afya na ugonjwa, mali na kutokuwa na mali hadi hapo kifo kitakapowatenganisha.

Hapa hatutaki kuangalia kama watu wetu wanakuwa kweli wameandaliwa na kama wanajua nini maana ya kuishi katika ndoa. Bila shaka suala hili tutalijadili mara nyingine kwa marefu na mapana yake stahiki.

WANASIASA:

Watu waume na wake walioamua kuingia kwenye shuguli za kisiasa hulazimika, kama ilivyo kwa wanandoa, kula kiapo na kuahidi kulinda na kutumikia kwa lengo la kuboresha maisha ya watu wetu. Wanasiasa pia husikika wakisema na tena kwa kutumia vitabu vitakatifu kuwa kwa akili zao timamu watailinda katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuwa wanaomba Mungu awasaidie katika utekelezaji huo.
Image by google

Kwa upande wa siasa nafahamu pia kuwa si wanasiasa wote wanaofahamu uzito na umuhimu wa kazi hii ya kitumishi. Kama asemavyo mwanafalsafa nguli John Locke kwamba mwanasiasa mzuri ni yule anayefahamu moyoni mwake kuwa kazi hiyo ni mkataba baina ya mwanasiasa na wananchi.

MADUDU

Pamoja na kula viapo wanandoa huvikiuka viapo vyao na kuvunja ahadi zao za ndoa na kuanzisha nyumba ndogo ambazo ni kinyume na ahadi zao za ndoa. Kama ilivyo kwa wanandoa, wanasiasa wetu wengi pia hukiuka na kuvunja ahadi na viapo vyao kwa kuchakachua rasilimali zetu na kushiriki kwenye ufisadi na wizi mkubwa mkubwa tu. Mfano wa uchakachuzi hapa ni pamoja na kushiriki katika ESCROW, EPA, RICHMOND na wizi mwingi unaowakesesha wananchi haki zao. Hivyo basi wanasiasa na wanandoa wote kwa nafasi zao hufanya madudu na kukiuka viapo vyao.

Thursday, November 19, 2015

German Universities Now All Free of Tuition Fees - Vyuo Vikuu Vyote Ujeruman Hakuna Ada sasa

Reichtag
Universities in Germany are now free of tuition fees for all including international students. Yesterday, Lower Saxony became the last of seven German states to abolish their tuition fees, which were already extremely low.
German universities had been charging for tuition since 2006. The measure proved unpopular, and German states began dropping them one by one. It is now all gone throughout the country, even for foreigners.
This means that now, both domestic and international undergraduate students at public universities in Germany are able to study in Germany for free, with just a small fee to cover administration– usually between €150 and €250 (US$170-280)  – and other living expenses costs per semester (food, transport, accommodation, entertainment, course materials and other necessities).
Germans barely had to pay for undergraduate study even before tuition fees were abolished. Semester fees averaged around €500 ($630). It is now gone.
Free education is a concept that is embraced in most of Europe with notable exceptions like the U.K., where the government voted to lift the cap on university fees in 2010, and tripled the tuition fees therefore. The measure has reportedly cost more money than it brought in. The Guardian reported last March that students are failing to pay back student loans.
Maybe for now, learning German might be the best financial choice an high school student can make.
Move to Germany with a student visa by using the step by step virtual assistant to the German student visa or reading about visa for international student in Germany on migreat.com.
Read more about Scholarships for Filipinos in Germany // Scholarships Para sa Mga Filipino sa Germany
Got questions about studying in Germany? Ask Migreat Communities in Germany.

TANZANIA YETU YA FURAHA - Atomic Jazz Band

Picha kwa hisani ya Google

Tanzania ni nchi ya aina yake na tuna wajibu wa kuifanya isonge mbele hasa. Atomic Jazz Band walifanya kazi hiyo vizuri kwa kutunga wimbo unaodumu daima. Wimbo wao utuhamasishe tutumie vyema vipaji vyetu ili tuijenge nchi hii.

Monday, November 16, 2015

A Nigerian Scholar Solves 156-Year-Old Mathematics Puzzle

Image courtesy of google
In what can be regarded as a rare achievement and possible entry in Guinness world of records, a Nigerian scholar, Dr Opeyemi Enoch, has successfully solved the 156 -year- old Riemann Hypothesis, the most important problem in Mathematics.
With this breakthrough, Dr Enoch, who teaches at the Federal University, Oye Ekiti (FUOYE), has become the fourth egghead to resolve one of the seven Millennium Problems in Mathematics.
The Kogi State-born mathematician had, before now, worked on mathematical models and structures for generating electricity from sound, thunder and Oceanic bodies.
A statement in Ado Ekiti, the Ekiti State capital yesterday, said Dr Enoch presentation of the Proof on November 11, 2015 during the International Conference on Mathematics and Computer Science in Vienna, Austria becomes more symbolic coming on the exact day and month 156 years after the problem was delivered by a German Mathematician in 1859.
The Riemann Zeta Hypothesis is one of the seven Millennium problems set forth by the Clay Mathematics Institute with a million Dollar reward for each solved problem for the past 16 years.
The statement reads in part, "Dr Enoch first investigated and then established the claims of Riemann. He went on to consider and to correct the misconceptions that were communicated by Mathematicians in the past generations, thus paving way for his solutions and proofs to be established.
"He also showed how other problems of this kind can be formulated and obtained the matrix that Hilbert and Poly predicted will give these undiscovered solutions. He revealed how these solutions are applicable in cryptography, quantum information science and in quantum computers."
Three of the problems had been solved and the prizes given to the winners. This makes it the fourth to be solved of all the seven problems.
Dr Enoch had previously designed a prototype of a silo for peasant farmers and also discovered a scientific technique for detecting and tracking someone on an evil mission.
Enoch has succeeded in inventing methods by which oil pipelines can be protected from vandalism and he is currently working on Mathematical approaches to Climate Change.
The home link to this story: http://allafrica.com/stories/201511160834.html?utm_campaign=trueAnthem:+Trending+Content&utm_content=564a324004d301547840c792&utm_medium=trueAnthem&utm_source=twitter

Saturday, November 14, 2015

What a Talent! Andrea Bocelli

Pourqoui Paris, Why Paris, Kwanini Paris?

Crowds in Paris
Picha kwa hisani ya BBC
Mwezi Januari mwaka huu 2015, dunia ishuhudia mauji ya wafanyakazi wa jarida la Charlie Hebdo jjijni Paris. Ufaransa na nchi nyingi za magharibi waliyaita mashambulizi hayo kama ni mbinu kuzuia uhuru wa kujieleza. Msingi ambao nchi nyingi zilizoendelea zinaona ni haki muhimu mno kwa binadamu na ambayo katu hakuna taifa lililostaarabika litakubali kuiacha haki hiyo ipotee. Hivyo nchi hizo hujinasibu kuwa zipo tayari kutumia gharama kubwa kutetea haki hiyo; ila tusisahau kuwa haki inafaa iendane na wajibu pia. Watu wengi tuliunga mkono wa wale ndugu wa lile jarida kwa maneno ya kifaransa #jesuisCharlie" kuwa mi ni Charlie ama nawaunga mkono wafanyakazi wa Charlie Hebdo.

Wakati Ufaransa na dunia kwa ujumla inaanza kusahau habari za mauji ya wafanyakazi wa Charlie Hebdo. Jiji lile lile la Paris linakutana na mashambulizi mauaji makubwa na ya kutisha mno ndani ya miezi kumi tu toka tukio la mwisho, ukiachia majaribio ya mashambulizi yaliyozimwa kwenye treni miezi ya hivi karibuni. Mashambulizi haya yameacha zaidi ya watu 120 waliopoteza maisha na mamia wengine wengi waliojeruhiwa.

media
Picha kwa hisani ya RFI
Ni dhahiri kuwa mauaji haya yanaacha maswali mengi kuliko majibu kwa sasa. Uchunguzi ukikamilika bila shaka tutafahamu vyema kuhusiana na mauaji hayo. Moja ya maswali yanayojitokeza ni kwanini ushambuliwe mji wa Paris? Kwanini Paris? Itafaa siku za usoni tuangalie watu na mfumo wa maisha ya Paris; linalosemekana kuwa moja kati ya majiji ya starehe zaidi duniani. Bila shaka Ufaransa itatumia uwezo na rasilimali zinazohitajika kupata kufahamu mengi zaidi juu ya hili na kuimarisha usalama duniani.

Kwa sasa tunasema poleni sana wakazi wa Paris na nchi ya ufaransa kwa ujumla. roho za marehemu waliofariki dunia wapumzike kwa amani, amina.

Saturday, November 7, 2015

Jina la Uwaridi - The Name of The Rose - Le Nom de la Rose






The Name of The Rose (Kiingereza), ll Nome Della Rosa(Kiitaliana), Der Name der Rose(Kijerumani), Le Nom de la Rose (Kifaransa) Jina la Waridi : Filamu nzuri mno. Filamu iliyoandaliwa toka kwenye kitabu tajwa hapo juu kilichoandikwa na mwandishi muitaliana Umberto Eco. Kitabu chake kinaeleza mambo anuwai ikiwa ni pamoja na namna ya kufumbua tatizo lililoigubika monastery moja ya wafransikani. Ndugu mdogo William wa Baskerville akisadia na mnovisi wake Christian Slater anasaidia kutoa ufumbuzi wa tatizo hilo kitaaluma, kiteolojia, kifalsafa. Anatumia mbinu za Aristotle, mafundisho ya kiteolojia ya Thomas wa Akwino na uwezo wake wa kiakili. Kwa hakika ni filamu nzuri mno. Wakati watengeneza filamu wetu wanaendelea kufanya kazi mbali mbali na kuandaa filamu wajifunze toka kwenye filamu nzuri kama hii. 



The Land of Riches and Opportunities


Image by google

Tanzania is a land of riches and indeed many opportunities and yet the country is counted among poor countries of the world. Tanzania is the home of the roof of the continent; mount Kilimanjaro, the country houses one of the world's natural wonders of Serengeti, Ngorongoro Crater, the beautiful islands of Zanzibar to mention but just a few... and Knud Vilby in his book  'Independent? Tanzania's challenges since Uhuru' writes on...

Image by the courtesy of google
"Tanzania is one of the most peaceful, stable and democratic countries in Africa. Nevertheless, the country faces almost insoluble problems. The African continent is one of a huge variety of difficulties and potentials. The problems of Tanzania tell us something about the huge challenges facing many other countries in the continent..."
e
o


Ngorongoro Crater
Part of the Zanzibar island

Nini Muhimu Zaidi Uchaguzi Mkuu?



Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa viongozi wa nchi yetu kuna mambo ambayo inafaa wanasiasa na wapiga kura tuyazingatie. Kuna maswali tunayopaswa kujiuliza:
1. Kwanini takwimu zinaonyesha uchumi unakuwa lakini bado kuna umasikini?
2. Vyama vituambie vitatumia mfumo upi wa uzalishaji mali? Je, ni ujamaa na kujitegemea,      Ubepari, Ubepari uchwara, ama mfumo upi?
3. Kuna jitihada zipi kupunguza kwa dhati umasikini mkubwa wa vijijini? (NBS 2012) inasema zaidi ya asilimia 70 ya watu wanaishi vijijini na kuwa karibu asilimia 90 ya watu hao ni masikini.
4. Miundo mbinu mibovu inatukosesha mapato mengi
    - Barabara vijijini mbovu hivyo usafirishaji mazao kupeleka sokoni inakuwa taabu
    - Reli ziboreshwe na kusafirisha mizigo mizito ili barabara zidumu muda mrefu na kupunguza ajali
5.Bandari ziboreshwe zaidi kupata biashara za nchi jirani
6. Elimu na wazazi wote wawasaidie vijana wetu kuongeza uthubutu, waongeze moyo wa kusoma vitabu zaidi kupata maarifa, wajifunze lugha za kishindani ili kushindana na vijana wenigne kote duniani
7. Watueleze watatumia vipi rasilimali nyingi zulizonazo kuondoa kabisa umasikini nchini. Tuna watu wengi (nguvu kazi), ardhi kubwa, bahari, maziwa, mito, jua (umeme jua), madini anuwai, gesi asilia, vivutio vingi vya utalii kwa uchache tu mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Ruaha, Mikumi, etc..Visiwa vya Zamzibar...

Baadhi ya viongozi wa siasa Tanzania wakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dar es Salaam,
31/08/2015

Thursday, October 29, 2015

AHADI ZA MTANZANIA


Google image

Chama cha TANU kilifanya kazi muhimu ya kuikomboa nchi yetu toka mikononi mwa wakoloni wa kiingereza. Haya yaliwezekana kutokana na uongozi thabiti wa kina J.K Nyerere, R.M Kawawa na viongozi wengine wazalendo, wenye utu na mapenzi makubwa kwa nchi na bara lao.

Malengo makubwa ya TANU ilikuwa ni kuleta uhuru wa waTanganyika na kushiriki katika ukombozi wa bara zima. Hapa tunakumbushana ahadi kumi za mwanaTANU ambazo zinafaa kuwa mwangaza kwa waTanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu na imani ya dini zetu. Na kwa nafasi ya kipekee ziwe mwangaza kwa viongozi popote walipo...

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.


Chanzo:http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/97717-ahadi-kumi-10-za-mwana-tanu-na-tanzania-yetu-ya-sasa.html

Wednesday, October 14, 2015

JULIUS NYERERE NA FIKRA IMARA

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1922-1999), waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru, rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika na kisha rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kiongozi wa kipekee sana kuwahi kutokea nchini Tanzania, barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.

Mwalimu Nyerere, alikuwa kiongozi wa kipekee kutokana na mitazamo, misimamo, na maamuzi yake. Ndugu huyu kamwe hakuwa malaika aliyeshuka toka mbinguni kuja kuishi nafasi la hasha! Huyu ni mwanadamu aliyetambua vipawa na uwezo wake na akavitumia vizuri kwa faida zake na kwa taifa aliloliongoza na kulipenda. Binadamu ni kiumbe cha kipekee mno. Tumeumbwa tukiwa na uwezo mkubwa kufanya mambo mengi yaliyo mapya kabisa, lakini wengi hatufanyi hivyo. Hatufanikiwi kwa kuwa hatuishughulishi akili yetu na vipaji vyetu kwa kiashi cha kutosha.

Katika makala haya naomuongelea kwa ufupi kabisa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoutumia uwezo wa kiakili kufanya mambo ambayo kamwe hayakuwa yamefanyika hapa nchini kwa jinsi yeye na viongozi wenzake walivyofanya. Naongelea sera za ujamaa. Hizi ni sera ambazo zimeandikwa na wanazuoni, wanahabari na watu anuwai kote duniani, wanaompenda na wanaomchukia Nyerere, wanaozipenda na wanaozichukia sera hizo.  

Ujamaa ilijengwa kwa dhana ya kihistoria, kifkra na kitaaluma ikiupinga ubepari kwa kuwa ulilenga kujenga jamii yenye furaha kwa kukandamiza kundi moja la watu ambapo wengi walifanya kazi kwa faida za mabwana wachache. Halikadhalika, iliupinga ujamaa wa kisanyansi kwa kuwa ulitaka kujenga jamii yenye furaha kwa njia ya mapigano. Mwalimu hakukubaliana na njia hizi katika kujenga jamii ya watu wenye kushirikiana, kupendana na kujitegemea.

Ujamaa uliotangazwa kupitia Azimio la Arusha, na ulishabihiana kifkra na baadhi ya siasa za Plato mwanafalsafa wa kale wa Kigiriki, mfano kwenye maadili ya uongozi kwa mwanasiasa. Ujamaa ulijengwa kupitia njia kuu mbili: utaifishaji wa njia kuu za uzalishaji mali binafsi na vijiji vya ujamaa. 

Utaifishaji wa njia kuu za uzalishaji mali kwa kiasi kikubwa kabisa ulichochewa na mfumo wa kibepari ambao Tanganyika iliupitia kwa takribani miaka sita 1961-1967. katika upepari huo wananchi wengi waliendelea kuishi katika umasikini mkubwa na kunyonywa kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Wananchi waliendelea kuvuja jasho kwa kuwafanyia kazi matajiri wale wale waliowafanyia kazi kipindi cha ukoloni. Kwa ufupi uchumi ulikuwa mikononi mwa Watanganyika matajiri na wageni wachache wenye asili ya Uingereza na bara Asia. Kwahiyo Watanganyika wa kawaida, wanafunzi chuo kikuu, wanaharakati wachache na Mwalimu walianza kuhoji kwanini walikuwa hawaoni tofauti ya kipindi cha ukoloni na kipindi cha uhuru. Uchumi huo wa kibepari uliongozwa na  misingi ya soko huru na huria ambapo serikali ya Tanganyika na baadaye Tanzania haikuwa na mamlaka juu yake. Hivyo ubinafsishaji lilikuwa ni suluhuhisho la msingi la kuanza upya. Jambo hilo halikuwa jepesi hata kidogo, lakini Mwalimu kwa mapenzi makubwa ya nchi yake alichukua uamuzi huo mgumu. 
Ubinafsishaji ulilenga kuipatia serikali uwezo wa kumiliki njia kuu za uchumi na kujaribu kujenga uchumi wa viwanda; uchumi ambao ungetoa ajira nyingi zenye staha kwa watanganyika na ambavyo vingetumia bidhaa ghafi toka mashamba ya Watanzania wenyewe. Mwalimu na wenzake walilenga pia kujenga taifa la kijamaa na MUHIMU hapa lenye KUJITEGEMEA, ndiyo maana njia nyingine ya kujaribu kujenga ujamaa ikawa ni kupitia vijiji vya ujamaa.

Vijiji vya ujamaa vililenga kuwaleta watu ili waishi pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana kama familia moja katika mashamba makubwa ya vijiji vya ujamaa. Na zaidi Wananchi walikusanywa kwa kuwa idadi ya watu ilikuwa ndogo na waliishi sehemu tofauti tofauti na mbalimbali ambapo ilikuwa vigumu kwa serikali kuwapatia huduma za kijamii. Kuhamia vijiji vya ujamaa ilikuwa hiari lakini baadaye nguvu ilitumika pale wananchi walipojivuta mno kutekeleza agizo hilo.

Sera za ujamaa na kujitegemea ambazo ziligusa nyanja zote za maisha yaani kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa kiasi fulani zilifanikiwa vyema na kwa kiasi kingine zilifeli vibaya. 

Kisiasa na kijamii jaribio la kujenga taifa la kijamaa lilifanikiwa sana. Mwalimu na wenzake walijenga taifa moja linaloundwa na zaidi ya makabila mia moja na ishirini. Walifanikiwa kuvunja kasumba za makabila makubwa na madogo. Walifanikiwa kushawishi watu wengi watumie lugha moja ya KISWAHILI, walifanikiwa kufanya watu waowane toka makabila na dini tofauti na zao. Kwa ujumla walifanikiwa kujenga moyo wa kindugu na mshikamano mkubwa baina ya watanzania. Kwenye huduma za kijamii nchi ilifanikiwa kupiga hatua kwenye elimu ya msingi ambapo watu wengi karibu wote walifanikiwa kujua kusoma na kuandika, huduma za afya pia zilikuwa nzuri na zilitolewa pia vyema bila ubaguzi. Kazi hii haikuwa ya Mwalimu Nyerere peke yake ni kazi aliyoifanya akishirikiana na viongozi wengine wengi kwa uchache tu hapa Abeid Karume, Rashidi Kawawa, Abdul Jumbe, George Kahama, Rupia, bibi Titi, Mwakawago na wengine wengi. Hata hivyo kiongozi mkuu alikuwa ni Mwalimu Nyerere. Kiongozi mwadilifu, imara na mpenda nchi huifanya nchi yake iwe na msimamo na kujijengea lulu na baraka za aina kwa aina kama amani na upendo miongoni mwa Watanzania. Kiongozi mkuu wa nchi akiwa mwadilifu, nchi hata kama ina matatizo bado ataweza kutoa mwelekeo mzuri kwa taifa lake.


Kiuchumi, jaribio la kujenga nchi ya kijamaa liliuharibu kabisa uchumi wa Tanzania. Nchi ilipoteza kabisa uwezo wake iliokuwa nao kabla ya kujaribu kuingia ujamaa. Uzalishaji wa chakula ulishuka, uzalishaji viwandani uliporomoka, bidhaa za matumizi ya kawaida kabisa kama mswaki, dawa ya meno, sabuni, nguo, unga viliadimika kabisa na uchumi kushuka chini kabisa. Hii ilichangiwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya Iddi Amini wa Uganda, mfumuko mkubwa wa bei za mafuta, ukame ulioikumba nchi, lakini hasa sera mbovu za uchumi zilizosababishwa na jaribio la kujenga uchumi wa kijamaa, hata hivyo hujuma toka kwa Waingereza, waliokuwa na hofu ya kusambaa kwa ujamaa kote Afrika Mashariki na hivyo kuleta athari kwenye mali zao hususani katika mabenki yao, nayo pia ilichangia kwenye kufanya jaribio la kujenga ujamaa lishindikane na uchumi uharibike kabisa.

Pamoja na shida zote hizo, Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa imara, mkweli, muwazi "mjamaa safi" ambaye kamwe hakujilimbikizia mali wala kuharibu rasilimali za taifa lake kwa manufaa binafsi kama tunavyoshuhudia hivi leo Tanzania na kote barani Afrika kwa baadhi ya wanasiasa wanavyofanya biashara kupitia dhamana ya vyeo walivyopewa na wananchi.

Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kujenga na kutumia fikra na vipaji vyetu vizuri kujinufaisha na hasa kuihudumia vyema jamii tunapoishi. Na kwa wenye nafasi ya uongozi popote pale toka katika ngazi ya familia tujenge uongozi bora na tuepuke ubinafsi tukifuata mfanowa Julius Kambarage Nyerere.

Martin Mandalu
Dar es Salaam,
14, 10, 2015

Monday, October 5, 2015

SIKU YA WALIMU DUNIANI

PG4A3893
Picha kwa hisani ya dewjiblog.com
Leo ni Siku ya Walimu Duniani. Ni siku mahususi kuwapongeza walimu kwa mchango wao mkubwa kwenye sekta zote za ujuzi. Kila mtaalamu duniani amepata mafunzo toka kwa mwalimu wa aina moja ama nyingine. Hakuna ujuzi hivi hivi bila kupitia kwa mtu anayeitwa mwalimu; hata wenye mlengo wa ujuzi, ama kupata elimu bila kutumia milango mitano ya hisia, hawawezi kulikwepa hili. Kwa mujibu wa "rationalists" kuna mambo ambayo tunaweza kuyajua kwa hisia tu. Hata kwa wadau hawa, lazima warejeshe shukrani kwa wazazi wao kama walimu wa mwanzo kabisa na hata kwa muungano mzuri wa chembe chembe hai za ubongo wao. Hivyo kwa ufupi kabisa, hakuna ujuzi bila mwalimu.

Tunaposherehekea ama kukumbuka siku hii kuna mengi ya kujiuliza. Mswali machache tu hapa; hivi mwalimu ana mazingira gani ya kufundishia; mazingira hayo ni salama na rafiki kwake? Je, hivi mwalimu aliye nguzo kubwa kwa ujuzi anapata stahiki zake kama inavyotakiwa? Je, huyu ndugu ana furaha ya kweli anapoifanya kazi yake? Walimu kote duniani wanakumbwa na shida na misukosuko inayowafanya washindwe kutekeleza majukumu yao vilivyo. Matatizo ya walimu yapo kwenye nchi zilizoendelea na zinazoendelea pia.

Kwenye baadhi ya nchi zilizoendelea, mwalimu anakutana na shida kubwa ya utovu wa nidhamu na maadili mabovu ya wanafunzi. Na nafasi ya mwalimu kuwarekebisha watoto imebanwa kwa kutumia lugha ya haki za watoto. Mwalimu hana nafasi wala mamlaka ya kumwadhibu mtoto kwa kuwa ni kinyume na haki za binadamu. Waingereza wana msemo wao, usipomchapa mtoto utampoteza. Hii ni tafsiri huru. Lakini Waingereza wenyewe na nchi nyingine zilizopiga hatua kubwa zaidi kimandeleo zina shida kubwa ya utovu wa nidhamu katika kundi la vijana ambao wanalindwa na haki za binadamu. Haki za binadamu ni muhimu kwa ustawi wa jamii lakini maadili na adhabu kiasi toka kwa mwalimu muhimu. Najua suala la kiasi ni gumu kulipima. Walimu wanakumbana pia na tatizo la tishio la usalama toka wanafunzi wenye silaha.

Katika nchi zetu zinazoendelea shida za walimu zipo za"kutosha" pia. Ni hivi karibuni tu walimu wa nchini Kenya ndiyo wamemaliza mgogoro wao na serikali. Miezi michache iliyopita walikutana na matatizo ya ukosefu wa usalama eneo la mpakani na Somalia. Nchini Tanzania walimu wana shida zao pia. Si lengo langu kuziorodhesha hapa hivi leo. Bali katika ukurasa huu, kwa maneno machache tu ni kutaka kukumbushia haki za walimu, kuhimiza uboreshwaji wa mazingira ya kufanyia kazi ndugu hawa ili wapate kufanya kazi kwa juhudi na maarifa zaidi kadri ya vipawa vyao.

Wasalaam,