Saturday, November 14, 2015

Pourqoui Paris, Why Paris, Kwanini Paris?

Crowds in Paris
Picha kwa hisani ya BBC
Mwezi Januari mwaka huu 2015, dunia ishuhudia mauji ya wafanyakazi wa jarida la Charlie Hebdo jjijni Paris. Ufaransa na nchi nyingi za magharibi waliyaita mashambulizi hayo kama ni mbinu kuzuia uhuru wa kujieleza. Msingi ambao nchi nyingi zilizoendelea zinaona ni haki muhimu mno kwa binadamu na ambayo katu hakuna taifa lililostaarabika litakubali kuiacha haki hiyo ipotee. Hivyo nchi hizo hujinasibu kuwa zipo tayari kutumia gharama kubwa kutetea haki hiyo; ila tusisahau kuwa haki inafaa iendane na wajibu pia. Watu wengi tuliunga mkono wa wale ndugu wa lile jarida kwa maneno ya kifaransa #jesuisCharlie" kuwa mi ni Charlie ama nawaunga mkono wafanyakazi wa Charlie Hebdo.

Wakati Ufaransa na dunia kwa ujumla inaanza kusahau habari za mauji ya wafanyakazi wa Charlie Hebdo. Jiji lile lile la Paris linakutana na mashambulizi mauaji makubwa na ya kutisha mno ndani ya miezi kumi tu toka tukio la mwisho, ukiachia majaribio ya mashambulizi yaliyozimwa kwenye treni miezi ya hivi karibuni. Mashambulizi haya yameacha zaidi ya watu 120 waliopoteza maisha na mamia wengine wengi waliojeruhiwa.

media
Picha kwa hisani ya RFI
Ni dhahiri kuwa mauaji haya yanaacha maswali mengi kuliko majibu kwa sasa. Uchunguzi ukikamilika bila shaka tutafahamu vyema kuhusiana na mauaji hayo. Moja ya maswali yanayojitokeza ni kwanini ushambuliwe mji wa Paris? Kwanini Paris? Itafaa siku za usoni tuangalie watu na mfumo wa maisha ya Paris; linalosemekana kuwa moja kati ya majiji ya starehe zaidi duniani. Bila shaka Ufaransa itatumia uwezo na rasilimali zinazohitajika kupata kufahamu mengi zaidi juu ya hili na kuimarisha usalama duniani.

Kwa sasa tunasema poleni sana wakazi wa Paris na nchi ya ufaransa kwa ujumla. roho za marehemu waliofariki dunia wapumzike kwa amani, amina.

No comments:

Post a Comment