Tunapoelekea uchaguzi mkuu wa viongozi wa nchi yetu kuna mambo ambayo inafaa wanasiasa na wapiga kura tuyazingatie. Kuna maswali tunayopaswa kujiuliza:
1. Kwanini takwimu zinaonyesha uchumi unakuwa lakini bado kuna umasikini?
2. Vyama vituambie vitatumia mfumo upi wa uzalishaji mali? Je, ni ujamaa na kujitegemea, Ubepari, Ubepari uchwara, ama mfumo upi?
3. Kuna jitihada zipi kupunguza kwa dhati umasikini mkubwa wa vijijini? (NBS 2012) inasema zaidi ya asilimia 70 ya watu wanaishi vijijini na kuwa karibu asilimia 90 ya watu hao ni masikini.
4. Miundo mbinu mibovu inatukosesha mapato mengi
- Barabara vijijini mbovu hivyo usafirishaji mazao kupeleka sokoni inakuwa taabu
- Reli ziboreshwe na kusafirisha mizigo mizito ili barabara zidumu muda mrefu na kupunguza ajali
5.Bandari ziboreshwe zaidi kupata biashara za nchi jirani
6. Elimu na wazazi wote wawasaidie vijana wetu kuongeza uthubutu, waongeze moyo wa kusoma vitabu zaidi kupata maarifa, wajifunze lugha za kishindani ili kushindana na vijana wenigne kote duniani
7. Watueleze watatumia vipi rasilimali nyingi zulizonazo kuondoa kabisa umasikini nchini. Tuna watu wengi (nguvu kazi), ardhi kubwa, bahari, maziwa, mito, jua (umeme jua), madini anuwai, gesi asilia, vivutio vingi vya utalii kwa uchache tu mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Ruaha, Mikumi, etc..Visiwa vya Zamzibar...
Baadhi ya viongozi wa siasa Tanzania wakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
31/08/2015
No comments:
Post a Comment