Maneno haya ya kiingereza juu ya rais huyu wa Marekani ni fundisho la aina yake tujifunze kupenda tunachofanya na tukifanye kwa moyo wote matokeo yake ni furaha na amani |
Huu unawafaa vijana wote ambao ni wepesi wa kukatishwa tamaa na watu wengine. Kumbuka hakuna mtu mwenye mamlaka ya kukufanya ukose furaha, ili ukose furaha, ukasirike ama uwe kwenye aina yote ya hisia ni lazima wewe mwenyewe uamue; Lincoln ni mfano mzuri mno. Maneno ya watu wengine si yenye kutubomoa.
Fundisho la pili ni kufanya kazi zetu kwa uadilifu, ubunifu, umakini na zaidi ya yote upendo. Mambo hayo husaidia kuvumbua mbinu mpya za kurahisisha maisha na kuleta maendeleo kwa watu haraka. Ndugu huyu japo si Mwafrika na atukumbushe kutenda mema!
No comments:
Post a Comment