Ndugu Ibrahim Badiri - Mtaalamu wa kikosi Cha zima moto Manispaa Mtwara-Mikindani akitoa mafunzo juu ya majanga hususani moto |
Katika mhadhara huo uliofanyika chuoni hapo, ndugu Badiri alisema watanzania wengi hawana elimu ya kujiokoa toka kwenye majanga na hivyo basi tatizo kama la moto linapotokea inakuwa vigumu kujiokoa.
Mtaalamu huyo alichanganua aina za moto: moto utokanao na mada za kioganiki, moto utokanao na hitilafu ya umeme, moto utokanao na gesi na moto utokanao na madini na vyuma mbalimbali. Kupambana na moto alisema kila aina ya moto huzimwa kwa kizima moto mahususi.
Moto wa vifaa vya kioganiki huweza kuzimwa kwa maji, poda / unga mkavu maalumu, mchanga
Moto wa umeme huzimwa kwa poda/unga mkavu maalum,
Moto wa gesi, kama ule wa kituo cha mafuta huzimwa kwa mchanga, poda / unga mkavu maalum
Moto wa madini huzimwa kwa poda/ unga mkavu maalumu.
Baadhi ya wana STEMMUCO wakifuatilia mafunzo hayo |
No comments:
Post a Comment