Hatimaye nimemaliza kusoma "The Innocent Man" cha John Grisham
Kitabu hiki kinajadili mambo mengi ya msingi mno kwa maisha ya binadamu. Mawili kati ya hayo ni; mosi jinsi ambavyo mfumo wa sheria, niruhusu kusema duniani, unavyoweza kuwa na mapungufu ya kutoa haki kwa binadamu, pili jinsi ambavyo watoa huduma wengine walivyo makini kuona haki inadhihirika na binadamu anatendewa haki katika mfumo wa sheria. Jambo la pili limenifurahisha sana!
sure, its a nice book to read
ReplyDeletesure, its a nice book to read
ReplyDelete