Success is never owned,
it is only rented and the rent is due every day".
Kitabu rejea;TAKE THE
STAIRS (7 steps to achieving true success).By Rory Vaden.
Katika maisha yetu
wanadamu kila mtu huwa anapenda kufanikiwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni kwenye
biashara,taaluma,ama ujuzi alionao.Ila watu wanashindwa kufahamau njia bora za
kufikia mafanikio yatakayowapa raha na furaha ya kudumu.Mafanikio yoyote
yanapatikana kwa hatua na si jambo lijalo kwa ghafla tu,na tatizo
linalowamaliza watu ni kuishi kwa kudhani mafanikio unaweza yafikia kwa mfano
wa kupanda lift ya ghorofa na punde ukajikuta umeshafika ghorofa ya tano,lakini
mafanikio hayapo hivo,mtu yeyote ukitaka kufanikiwa ni lazima upande
ngazi(hatua) ili uende hatua kwa hatua,labda jiulize swali dogo tu je, upandapo
lift katika ghorofa mwili wako huwa unapata faida ipi? ,hebu mtazame mtu
apandae ghorofa kwa kutumia ngazi,mtu huyu hupata faida nyingi ,kwanza mwili
wake unapotoa jasho huujenga na kupunguza sukari isiyotakiwa mwilini na
faida nyingine kadha wa kadha.Huu ni mfano tu wa ngazi za kupanda katika
jengo,basi ndivyo yalivyo na mafanikio ya mtu huwa yanahitaji kuyaendea
kwa kufuata hatua ili uweze kuwa na uchungu nayo pale ukishayapata,jitoe mapema
kwenye ESCALATOR MENTALITY ili usizidi kuupoteza muda.
Mafanikio ya mtu
yeyote yanajengwa kwa mtu kuwa na nidhamu kubwa na si kwa njia za mikato kama
watu wadhaniavyo.Kuwa na nidhamu binafsi (self discipline) si jambo jepesi hata
kidogo,uonapo watu wamefanikiwa jua kwamba walitengeneza nidhamu zao
binafsi,hawakungoja kusukumwa sukumwa katika kutenda yale wapendayo kuyatenda
na ndipo walijikuta wakifika kule walipotamani kufika.Mpendwa msomaji nikuambie
tu wazi,utakapo amua leo kujijengea nidhamu binafsi jua si jambo ambalo
utalipata kwa wakati mfupi na pia hutalipata kwa gharama ndogo,jipange kujitoa
kwelikweli ili ujijengee nidhamu binafsi katika kazi yako,biashara yako,kipaji
chako n.k.
Pia watu wengi hupenda
na hutamani kufikia hatua kubwa za mafanikio lakini sumu kubwa inayowamaliza ni
tabia ya kupenda kuhairisha mambo.Unakuta mtu anatamani kuwa mfanyabiashara
mkubwa lakini kila siku husema nitaanza kesho Mwandishi mmoja alisema
"successful people form the habit of doing things that failures don't like
doing".Na hivi ndivyo watu wakubwa wanavyofanikiwa ni kwa sababu
hawaghairishi mambo na nidhamu zao za hali ya juu ndizo zinazowasaidia kuviishi
viapo vyao.
Lakini pia watu
hudhani watu waliofanikiwa walikutana utajiri wa kifedha,kuwa na biashara
kubwa,ama ubobezi katika fani fulani kwa siku moja,lakini si kweli,ukirudi na
kufuatilia watu wote waliofanikiwa walipita maisha ya kufanya mambo madogo
madogo yaliyo na tija katika maisha yao na baadaye wakajikuta yakiwaletea
matokeo makubwa(small choices yield big results),anza kujijengea nidhamu katika
mambo madogo madogo nawe utajishuhudia ukipiga hatua siku baada ya siku.
Ukiwa na nidhamu
maishani utaishi maisha unayoyapenda ikiwa ni katika biashara yako,katika kazi
yako au ujuzi wako na maisha hayo ya furaha hayatakuwa ya muda bali
yatakuwa ni ya kudumu maishani mwako,kumbuka kuwa mafanikio hayana
umiliki wa kudumu ni kama kitu kilichokodishwa tu na gharama yake ya kulipia ni
nidhamu.Ikiwa unataka uwe na afya bora lazima uwe na nidhamu katika ulaji
wako,ukiwa unataka mafanikio ya kibiashara ni lazima uwe na nidhamu katika
biashara yako,ukiwa unataka ndoa yako iwe yenye furaha lazima uwe na nidhamu
katika ndoa yako n.k.
Nenda kafanyie kazi
haya machache niliyokushirisha ukilianza vyema juma hili la 41 katika mwaka
wetu 2018,na nitaendelea kukushirikisha hatua 7 saba muhimu za kufikia
mafanikio yoyote makubwa,njia hizi amezielezea vyema mwandishi Rory
Vaden.Nikutakie heri wewe unaeenda kuchukua hatua ya kuyafanyia kazi yale
ambayo umejifunza.
Na mwanafunzi wa
kudumu wa shule ya maisha, Mchambuzi wa vitabu na Mshairi;
Marko Kinyafu.
+255 714 129 520.
Dar es
salaam,Tanzania.
Kupata maarifa ni bure
ila kulipa gharama ya ujinga ni kazi kubwa kuliko gharama unayoikimbia sasa ya
kupata kile kilichobora kwa ukombozi wa fikra zako.