Saturday, June 18, 2016

TAFAKARI 40 KWA YESU WA EKARISTI TAKATIFU


Ni kitabu mahususi kwa kutoa msaada na mwongozo wa namna ya kumwambudu Yesu Kristo wa Ekaristi Takatifu.

Kitabu hiki kinamlenga kila mwamini anayemtambua na kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu, Mwokozi wa maisha yake, na nafsi ya pili ya Mungu. Kwahiyo basi, kinawalenga watu wa marika yote; watoto, vijana, watu wa makamo na wazee.

Kuna jumla ya tafakari 40 ambazo zote kila moja kwa namna yake zinaongelea maisha ya Yesu katika mahusiano na wanadamu na baba yake, ambaye ni baba yetu pia. Kitabuni kuna virutubisho vya kiroho vya kila namna, japokuwa msisitizo ukiwa ni juu ya kumwabudu Yesu Kristo.


Kitabu hiki kiliandikwa na Dominique Nothomb (22 Juni 1924 - 9 Novemba 2008) Padre wa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers - M.Afr). Na tafsiri ilifanywa na Martin Mandalu Mlei wa Jimbo Katoliki Mtwara.

Kitaanza kupatikana hiki karibuni katika maduka ya vitabu. Unaweza kupata nakala yako pia kwa kuwasiliana nami kwa nambari +255767864379 ama +255715864379

No comments:

Post a Comment