Thursday, April 16, 2015
Wednesday, February 4, 2015
TUMIA FURSA VYEMA NJE YA NCHI YAKO
Na. Theddy Matemu Sawaki
Fursa zipo kila sehemu - This image for education purpose is taken from another website |
Tofauti na
elimu ya darasani lakini mambo ya elimu dunia Zingatia yafuatayo.
Ø Kujali muda.
Ø Kuheshimu kila mtu.
Ø Kujituma.
Ø Kujifunza lugha na tamaduni
za wenyeji.
Ø Kuwa msikilizaji zaidi
ya msemaji.
Ø Kuwa tayari kupokea
ushauri toka kwa watu wote hata wa kada za chini.
Nimekuwa nikizunguka kwenye mitaa ya Mji wa
Tokyo nikaja kugundua wahindi ni watu wanaojua kucheza na fursa wanazozipata.
Sio kwa nchi zinazoendelea tu hata kwa nchi zilizoendelea kama Japani.
Na
nikaamini kuwa darasani tu haitoshi kukufanya ukapata maendeleo ya Kimaisha.
Kwa kuwa napenda kula nimekuwa nikizunguka katika mitaa ya Tokyo kutafuta
chakula ninachokipenda. Nimekutana na migahawa ya Kijapani na kihindi na
kitaliano.Migahawa ya kihindi ina sehemu ndogo sana ya kufanyia biashara
naamnisha ukubwa wa nyumba maana jiko liko hapo hapo na viti vya kulia wateja
viko hapo hapo karibu( ila kwa huku wamejitahidi kwa usafi sio kama
wanavyoutufanyia kwetu Tanzania)hapo napo ni kipengele kingine
cha kujifunza kumbe kuwa wasafi wanaweza isipokuwa ni namna gani nchi husika
inajali wananchi wake.
Katika
kufanya utafiti wangu wa kichumi usio rasmi (mimi sio mwana uchumi) nikagundua
wahindi wameweza kujenga umaarufu katika biashara ya chakula na wana wateja
wengi sana wenyeji wa Japani. Nikamwuliza mmoja wa wenye migahawa wa kihindi
umewezaje kufanikiwa katika kupata wateja wengi akaniambia nina miaka 30 hapa Japani
na kweli anaongea kiJapani kama amezaliwa nacho.
Kwanza
kabisa alipofika hapa alijifunza lugha (naweza sema kwa Japani ili uweze kuishi
vizuri ni vyema ujue lugha vinginevyo utapata shida katika huduma za muhimu),pia
alijifunza tamaduni na mengine muhimu katika maisha ya waJapani. Hii ilimsaidia
kuweza kuwasiliana na wateja wake, kujua nini wanapenda na nini hawapendi kujua
jinsi gani angeweza kuwafanya wafurahie huduma zake. Haya yote alifanikiwa pale
alipoajiri wafanyakazi wa kijapani wakati akianza biashara yake na kuwafundisha
jinsi ya kuandaa vyakula vya kihindi nao wakamfundisha lugha na mengine yote ya
muhimu.
Alipoona
biashara imeshamiri alipunguza wafanyakazi wake. Baada yakupunguza wafanya kazi
biashara ikayumba sana. Akaitisha kikao na wafanya kazi wake waliobaki kutaka
kujua tatizo ni nini kama unavyojua wafanyabiashara wengi wa kihindi hupenda
kuamrisha zaidi na huamini watu wachache tu.
Mmoja
wa wafanyakazi akamwambia bosi ili biashara ikue warudishe wale wafanyakazi
uliowapunguza kwasababu wanajua siri ya kazi na wameizoea na ndio walichangia
biahara kukua. Hapo ndipo alipojifunza kwamba ili upate mafanikio lazima uamini
kwamba kila mtu hata kama ni mdogo kiasi gani anaweza kuwa na mchango katika
maisha yako. Muda mfupi baada ya wale wafanyakazi kurudishwa kazini biashara
ikainuka mpaka leo na wateja wanajaa mpaka wanasubiria nafasi ya kuketi kwa
foleni.
Nimejifunza
Maisha sio kukaa darasani tu bali pia na hasa namna gani unaweza kuthubutu na
kufanya chochote hata kama ni nje na nchi yako na ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa
sana, ili mradi kuwe na amani na utulivu katika nchi husika.
Saturday, November 15, 2014
MAISHA NI NINI? - What is Life? - Qu'est-ce que la vie?
Image by google |
Hivi karibuni nimesikia kutoka radio Maria Tanzania kuwa wana mpango wa kuanzisha kipindi kipya juu ya maisha. Nimesikia wanauliza maisha ni nini? Swali hilo limenivutia kufanya tafakari. Kisha tafakari hiyo nikaona vyema kuwashirikisha watakaopata fursa ya kutembelea ukurasa huu.
Maisha ni nini? Ni swali linalohitaji kufikiria ili kulijibu na hakika mtu hawezi kutoa jibu la maana kama atafanya hivyo bila tafakari. Swali hili lahitaji maelezo ya utangulizi kabla ya kueleza maana ya maisha. Maisha yanahusu viumbe hai, swali letu linamlega hasa binadamu nami nitamuelezea binadamu bila kwenda kwenye falsafa ya ndani ya binadamu - philosophical anthropology, nitamuelezea binadamu kwa lugha nyepesi kabisa ili kila msomaji aelewe. Hivyo basi kwa kuanza na kiumbe huyu, binadamu ni kiumbe mwenye akili na utashi zaidi kuliko viumbe wengine.
Kiumbe huyu huanza safari ya maisha baada ya mtu mume na mtu mke kushiriki tendo la ndoa na kutungwa mimba. Kisha kutungwa mimba kiumbe kipya kinaanza kuishi ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke. Kuishi kwa kiumbe ndani ya mwanamke kunatupatia fursa ya kurudi kwenye swali letu la msingi la maisha, yaani maisha ni nini hasa?
Maisha ni jumla ya shughuli zote azifanyazo binadamu toka kutungwa mimba hadi pale moyo (kiungo chenye kazi ya kusukuma damu mwilini sehemu zote za mwili na hivyo kuurutubisha mwili kwani damu ndiyo njia kuu ya usafirishaji mwilini) utakapokoma kufanya kazi yake.
Katika maisha ya kila binadamu kuna shughuli zinazofanana kwa viumbe wote na kuna shughuli zinazotofautiana toka binadamu mmoja hadi mwingine. Kwa kawaidaa shughuli zote za kimaumbile za binadamu hufanana. Shughuli hizo ni pamoja na zile zifanyikazo ndani ya mwili wa binadamu; ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo zaidi ya kumi inayoshirikiana kati yao na pia ikipata ushirikiano na idara kadhaa mwilini. Baadhi ya mifumo iliyo mwilini kwa binadamu ni pamoja na mfumo wa usafirishaji ambapo moyo na mishipa mwilini husafirisha damu na vyakula sehemu zote za mwili. Upumuaji ni mfumo unaotumia idara za pua, mapafu na kadhalika kuwezesha upumuaji wa mwili. Utoaji taka mwilini huhusisha idara kadhaa na hata mifumo mingine kufanya kazi hiyo...
Pamoja na shughuli zinazofanana kwa binadamu wote kuna mahitaji ya lazima ambayo ni muhimu kwa viumbe wote hao bila kuzingatia nafasi zao kijamii, kiuchumi na kadhalika. Chakula, hewa safi, na hifadhi ya namna fulani ni kati ya mahitaji ya lazima kwa binadamu wote.
Ili aweze kuishi vyema na mwili wake ufanye kazi, binadamu analazimika kula; lazima apate chakula katika kipindi fulani ili mwili wake uendelee kupata mahitaji na virutubisho vinavyouwezesha mwili kuendelea kuishi, hali kadhalika kwa hewa safi. Ili mwili uendelee na kazi zake lazima upate hewa safi ili kubadilishana kwa hewa safi (Okisijeni O2) na hewa chafu (Kaboni diokisaidi CO2) kuendelee kufanyika. Binadamu wote huhitaji hifadhi ya namna fulani; toka kwenye mavazi hadi nyumba ya kujihifadhi, ni ubora tu ndiyo hutofautiana toka mmoja hadi mwingine.
Tunapojiuliza maisha ni nini kuna jambo la lazima kuligusa pia. Nini lengo la maisha? LENGO KUU LA MAISHA NI KUTAFUTA FURAHA. Kwenye dini tunaambiwa lengo kuu la maisha ni kumtumikia Mungu kupitia huduma kwa binadamu wenzetu na mwisho turudi kwa Mungu. Kwahiyo, kwa mara nyingine, kwa binadamu wote lengo kuu la maisha ni kutafuta furaha. Binadamu wote shughuli zetu zote, ama kwa kujua ama kwa kutokufahamu, ni harakati za kutafuta furaha na hivyo basi maisha ni jumla ya shughuli zote binadamu anazozifanya katika harakati za kusaka furaha.
Binadamu wote bila kasoro, lengo la maisha yetu ni kusaka furaha. Tuliona mwanzoni kuwa binadamu ni kiumbe mwenye akili na utashi mkubwa kuliko viumbe wengine wote. Utashi na akili nyingi aliyonayo binadamu humpatia fursa ya kuitafuta furaha kwa namna ya kipekee kwa jinsi ya maumbile na muundo wake unaotokana na mpangilio wa 'genes' zake, ushawishi wa mazingira aliyolelewa na pia aina na ubora wa chakula alacho hasa toka utotoni. Ndiyo maana kuna wenye hutafuta furaha kwa kufanya kazi halali kwa bidii, wengine kwa kufanya kazi haramu kwa bidii (kazi haramu huleta furaha ya muda tu kwa kuwa huwadhuru binadamu wengine), wengine kwa namna yao kulingana na vipaji vyao na wengine kwa namna zao kwa namna namna.
Hivyo basi maisha ni jumla ya shughuli zote azifanyazo binadamu katika harakati za kusaka furaha katika kipindi chote ambapo moyo unafanya kazi ya kusukuma damu mwilini!
Martin Mandalu
Alice, Eastern Cape
15/11/2014
Martin Mandalu
Alice, Eastern Cape
15/11/2014
Wednesday, November 5, 2014
BETTER LOOK?
One World Trade Center as by wikipedia |
World Trade Center before destuction. Image by abazon blog |
Thursday, October 16, 2014
Wasomi wahoji kwa nini Mwl Nyerere ahujumiwe? Ni katika Tuzo ya Nobeli, Ulaya watiliwa shaka
UTOAJI wa Tuzo maarufuna muhimu za Nobeli kwa watu mashuhuri na wenye mafanikio ya kipekee katika
maendeleo na amani ya dunia umeanza kutiliwa shaka na baadhi ya wasomi barani
Afrika, na hususan wanazuoni katika baadhi ya vyuo vikuu Kusini mwa Jangwa la
Sahara, Raia Mwema, imebaini.
Mijadala ya chini chini
imeanza kurindima miongoni mwa wanazuoni, wakihoji kulikoni Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa kiungo katika ukomboni barani Afrika na hata
kushiriki kuratibu harakati za vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini,
asipewe tuzo ya amani.
Wakati tayari tuzo hizo
zimekwishatolewa kwa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, mwaka 2011, kwa
kupigania haki za wanawake ili washiriki kujenga amani, aliyekuwa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, mwaka 2001, Askofu Desmond Tutu na Nelson
Mandela, hoja zimeanza kuibuka kwa nini si Mwalimu Nyerere?
Wasomi hao sasa wanakosoa
tuzo hizo na kudai kwamba Mwalimu ananyimwa kwa sababu aliyapinga mataifa ya
magharibi alipokuwa akiongoza harakati za kudai uhuru kusini mwa nchi za Afrika
na akishiriki kuunganisha nchi hizo, sambamba na kutetea haki za binadamu,
akiwa kiongozi aliyeishi kwa mfano mbele ya raia wake.
Wengi wanaamini Mwalimu
ni kiongozi wa mfano katika kuthamini usawa wa binadamu jambo ambalo ndilo
msingi wa amani ya dunia na kwa hiyo, alistahili kutunukiwa Tuzo ya Amani ya
Nobeli.
Tuzo hizo zilizoanzishwa
na raia Norway, hutolewa na kutambulika kimataifa ili kuwapa heshima watu
mashuhuri waliosaidia dunia katika nyanja mbalimbali za uchumi, amani, fasihi
na masuala ya sayansi kama fizikia, kemia, hisabati na mengineyo.
Wahadhiri wakosoa
Mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM), chuo ambacho Mwalimu alikianzisha na mara kwa mara
kufika hapo kwa ajili ya mijadala na wanafunzi kuhusu uhuru na maendeleo ya
Afrika na dunia kwa ujumla, Bashiru Alli, anaamini Mwalimu anastahili tuzo hiyo
lakini ananyimwa kutokana na kuyaudhi mataifa ya magharibi wakati aliongoza
harakati za kudai haki za binadamu na uhuru wa mataifa ya Afrika.
“Kuhusu maoni yangu juu
ya namna baadhi media (vyombo vya habari), wanazuoni na watu mashuhuri wa nchi
za magharibi wanavyopuuza mchango wa Mwalimu katika medani za mfumo wa siasa
uchumi duniani na siasa za mahusiano ya kimataifa. Maoni yangu ni kwamba
Mwalimu alikuwa mpinzani mkubwa wa mifumo yote kandamizi hususan mfumo dume,
ukaburu na ubeberu.
“Upinzani wa Mwalimu
dhidi ya mifumo hii ulimjengea heshima miongoni mwa wanyonge duniani kote, vile
vile alikuwa na maadui wengi ingawa maadui wake hawakufanikiwa kuutoa uhai wake
kama ilivyotokea kwa Patrice Lumumba wa Congo.
“Hata kama Mwalimu hakuwa
mmoja wa washindi wa Nishani ya Amani ya Nobel kama vile Neslon Mandela, lakini
mchango wake katika mapambano ya ukombozi hasa barani Afrika hauwezi kupuuzwa.
Hata kama mchango huo wa Mwalimu hautangazwi sana na vyombo vingi vya habari
vya magharibi au wasomi wengi wa nchi za Magharibi lakini maandishi yake,
hotuba zake na msimamo wake dhidi ya dhuluma, unyonyaji na ukandamizji ni
urithi usiokifani wa dunia. Sio rahisi urithi huu wa dunia hauwezi kupotea hivi
hivi,” anasema Mhadhiri Bashiru Alli.
Mhadhiri mwingine wa Chuo
Kikuu cha Stefano Moshi Memorial, Dk. Gaspar Mpehongwa, anasema vyombo habari
vya nchi za magharibi havikuwahi kumpa nafasi Mwalimu Nyerere kwa sababu
alikuwa “mwiba” kwa mataifa ya magharibi kutokana na hatua yake ya kukosoa kila
mara, sera zao za kibepari na ukoloni mambo leo dhidi ya nchi masikini za dunia
ya tatu.
Alisema kuwa sera za
Mwalimu za Ujamaa na Kujitegemea ziliendana na zile za mataifa ya na nchi za
kikomunisti za China na Urusi, hivyo mataifa ya Ulaya Magharibi yenye kufuata
sera za kibepari na uchumi huria yalimtenga.
“Mwalimu alikuwa black
listed na mataifa ya Ulaya Magharibi na Marekani kutokana na kuegemea zaidi
katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na hata vyombo vyao vya habari havikuwahi
kumsema vizuri,” alieleza Mhadhiri huyo.
Alisema Mwalimu Nyerere
alipinga sera hizo hasa Shirika la Fedha la Dunia(IMF) na Benki ya Dunia (WB)
taasisi ambazo zililenga kukandamiza nchi masikini hasa za dunia ya tatu,
Tanzania miongoni.
“Kwa bahati nzuri pamoja
na changamoto hiyo ya nchi za Ulaya Magharibi Mwalimu aliendelea kutambuliwa
kama moja wa mashujaa wa Afrika ambao walipigania maslahi ya nchi zao mbele ya
Jumuiya ya Kimataifa”
“Afrika iliheshimika sana
wakati huo kutokana na kuwa na viongozi wenye mtazamo chanya katika masuala ya
kiuchumi, kijamii na kisiasa tofauti na viongozi wa sasa ambao huitikia na
kucheza kila wimbo kutoka taasisi za Bretton Woods (mfumo wa kibiashara na
kifedha wa mataifa makubwa),”aliongeza.
“Kwa mfano leo hata
ukitaka uongozi wa umma vigezo vinavyotumika ni fedha badala ya uwezo wa mtu na
tabia hii imesababisha kuwa na aina ya viongozi katika sekta za umma
wanaojilimbikizia mali na madaraka,” alisema Mpehongwa.
“Na factor (kigezo) ya
uongozi ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi angalia mfano nchi ndogo kama
Uswisi imeendelea kutokana na uongozi thabiti lakini Tanzania yenye rasilimali
nyingi kuliko Uswisi imeendelea kubaki kuwa moja ya nchi maskini na serikali
yake inajiendesha kwa kutegemea hisani ya nchi za Ulaya,” alisema.
Kwa upande wake,
Mwananahabari mkongwe na mwandishi wa vitabu nchini, ambaye baadhi ya vitabu
alivyoandika ni pamoja na “Harakati za Nchi zilizo Mstari wa Mbele na Unyanyo
wa Julius Nyerere,” Mkwabi Ng’wanakilala, anasema inawezekana kwa mfano, Nelson
Mandela na Mwalimu Julius Nyerere walikuwa katika mizani tofauti ya kimtazamo
na kwamba ndiyo sababu inayowafanya wapate heshima tofauti hasa kwa watu wa
Magharibi.
Kwa upande wa Nelson
Mandela, anasema, hali yake ilikuwa ngumu kwa sababu hakuwa anafukuza wakoloni
isipokuwa alikuwa anapigania maslahi sawa ya Waafrika Kusini weusi dhidi ya
makaburu, wakati kwa upande wa Nyerere kazi ilikuwa ni kuwafukuza wazungu
waondoke Tanganyika.
“Mandela alionekana kama
mtu ambaye hatakuwa na madhara makubwa kwa uwekezaji na maslahi ya wazungu na
makaburu Afrika Kusini, walijua wanaweza kumpa anachotaka bila kupoteza
chochote, na ndiyo hali inavyoonekana mpaka leo, Waafrika weusi bado wana hali
ngumu kiuchumi kama ilivyokuwa wakati ubaguzi,” anaeleza.
Anafafanua kuwa pamoja na
kwamba Mandela ni mpigania uhuru na ukombozi wa Afrika na amekaa jela miaka 27
kwa ajili ya kupigania ukombozi wa mtu mweusi, lakini ni kama nchi za Magharibi
zilimtumia kimkakati kwa mantiki kwamba anaweza akawafanya wakaishi kwa amani
kwa kuwa atakubalika na wote, weusi na makaburu.
“Hata ukiangalia release
(kuachiwa toka jela) yake ni kama ilikuwa staged (ilipangwa kimkakati) ili
kuweza kukidhi matakwa yao kutokana na shinikizo lilikuwapo wakati huo, na
walipomwachia amekuwa Rais na haki za weusi kupiga kura na mambo mengine
wamepata lakini kwa kweli bado kiuchumi hali haijabadilika sana ni kama ile ile
tu” anasema.
Anasema kuwa huyu ni
lazima asifiwe kwa kuwa ni mtu ambaye hana madhara makubwa sana kwao, kuendelea
kumsifia ni kujihakikishia kuendelea kujiimarisha katika hali waliyo nayo
tofauti na Mwalimu Nyerere.
Kwa upande wa Mwalimu
Nyerere anasema alikuwa anataka uhuru kamili katika nyanja zote, na alikuwa
anawaambia ukweli bila kujali watamtafsiri vipi, na kwamba ilifikia kipindi
wakaumuona kama mkomunisti lakini kimsingi hakuwa mkumnisti yeye alibaki kuwa
mjamaa hata kama alikuwa na marafiki China na Cuba.
“Mwalimu kama ilivyokuwa
kwa Nkrumah walitaka kuvunja vunja kabisa mizizi ya unyonyaji, wamchukia kwa
sababu ya impact (matokeo) ya misimamo yake, he was very disturbing (alikuwa
msumbufu sana) kwao, haikuwa rahisi kumfanyaia ujanja ujanja” alisema.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Dk. Charles Kitima, anasema kuwa
Mwalimu Nyerere hawezi kuwa maarufu na kusifiwa na watu ambao aliongoza juhudi
za kuwakatia mirija ya kunyonya rasilimali za Afrika.
Anasema Mwalimu Nyerere
aliongoza juhudi za nchi zilizo mstari wa mbele kwa kuwaunganisha Waafrika
kupinga aina zote za unyonyaji wa wakoloni na koloni mamboleo kitu ambacho
hakikufurahiwa na wakubwa wengi wa Magharibi.
“Asingeweza kuwa maarufu
kwa watu ambao aliwanyang’anya ulaji, kumbuka ni juhudi zake ndiyo
ziliwaunganisha Waafrika nay eye akawa Mwenyekiti wan chi zilizo mstari wa
mbele kuwapinga hawa,kwao mtu wa namna hi hawezi kuwa shujaa hata siku moja”
alisema.
Anasema kwa Afrika kwa
kiasi kikubwa inajitahidi kumkumbuka na kumuenzi ambapo sasa baadhi ya nchi
kama Rwanda wana maadhimisho rasmi ya kumuenzi Mwalimu na Umoja wa Afrika
umeanzisha Scholarship kwa heshima ya Mwalimu.
Mwalimu Nyerere African
Union Sholarship Scheme imeanzishwa kwa ushirkiano na India kuwasomesha Wanafunzi
wa Afrika katika vyuo mahiri Afrika, katika fani ya sayansi na teknolojia kwa
ngazi za shahada, shahada za uzamili na uzamivu.
Chuo Kikuu cha Edinburgh
ambako Mwalimu alichukua shahada yake ya uzamili mwaka 1949, kilianzisha The
Julius Nyerere Master’s Scholarship mwaka 2009, kwa ajili ya wanafunzi wa
Tanzania kusoma katika chuo hicho.
Dk. Kitima anasema kuwa
sababu nyingine ambayo inafanya Mwalimu asipate heshima hiyo ni jinsi serikali
inavyosimamia masuala ya msingi aliyoyaanzisha, kwamba udhaifu huo ndiyo
unafanya hata watu wengine wasione mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Afrika
huru.
Ameshauri ni muhimu
serikali kurejesha somo la historia shuleni ili wanafunzi wajifunze historia ya
nchi yao na kuwatambua mashujaa wao na hapo ndipo wanaweza kusimama kidete na
kuitetea hadhi ya taifa lao.
Naye Mwanasheria Edward
Lekaita alieleza kuwa mataifa ya magharibi pamoja na vyombo vya vya habari
hayakuweza kutambua mchango wa Mwalimu kutokana na tabia yao ya kujali masuala
yenye maslahi na mataifa yao.
“Vyombo vya habari vya
magharibi siku zote ajenda yao kubwa ni kuandika habari zenye maslahi na
mataifa yao hasa habari nyingi za mataifa masikini Afrika na yale ya Bara la
Asia”
“Walikuwa double standard
(ndimi mbili) katika masuala mengi ya msingi kwa mfano walitambua umuhimu wa
Nelson Mandela baada ya kutoka gerezani na kuioongoza Afrika ya Kusini huru
lakini kabla ya hapo walimtabua kama gaidi.”
Alisema Mwalimu na
wenzake kama Nkwame Nkrumah wa Ghana, Nelson Mandela wa Afrika ya Kusini,
Lepold Senghor wa Senegal walijitahidi kuwaunganisha wananchi ili kuondoa
ukoloni na ubaguzi katika nchi zao.
“Ni aibu mambo
yanayofanyika sasa ni kinyume na dhamira iliyowasukama viongozi wetu wa zamani
kupigani uhuru kutoka kwa wakoloni hata wakati mwingine kuhatarisha maisha yao”alisema.
Kwa upande wao, baadhi ya
wakazi wa Mbeya waliozungumza na mwandishi wetu wanamueleza Nyerere kama
masikini jeuri, kwamba katika harakati zake za kupigania haki na utu kwa
wanadamu wote hakujali mabavu ya mataifa makubwa wala uwezo wao mkubwa kifedha.
“Nyerere alikuwa masikini
jeuri, alikataa kufanya biashara na Makaburu wa Afrika Kusini, hatua
inayotugharimu hadi leo, lakini heshima ya msimamo wake tunavivunia hadi leo,”
anasema mkazi wa jiji hilo, Newton Kyando.
Kyando anatoa mifano
zaidi kuonyesha ujasiri wa Nyerere kupigania haki za wanyonge duniani,
akikumbuka namna Mwalimu alivyokataa kuitambua serikali ya Mlowezi Ian Smith,
alipojitangazia uhuru wa Zimbabwe, wakati huo ikijulikana kama Northern
Rhodesia. Mbali na uamuzi huo, Nyerere akipata kuvunja uhusiano na Israel
akipinga uonevu dhidi ya wananchi wa Palestine.
“Nyerere alivuka mipaka
ya dini, alikuwa mkristo safi, tena mkatoliki, lakini alivunja uhusiano na
Israel kupinga uonevu dhidi ya Wapalestina ambao wengi ni Waislamu, alichokizingatia
yeye ni haki za wanyonge na utu wa mtu,” anasema Kyando kisha anaendelea
akisema, “Pamoja na Chama cha ANC cha Afrika Kusini kilitangulia kuanzishwa,
ilikuwa ni TANU iliyokijenga kufikia pale ilipofikia leo hadi kufanikiwa
kupatikana kwa uhuru wa Afrika Kusini, na unapotaja TANU unamtaja Mwalimu
Nyerere,” anasema Kyando.
Wananchi hao wanakumbuka
pia mchango wa Mwalimu Nyerere kwenye medani ya kimataifa, ikiwamo kuwa msemaji
wa “South South Commission,” pamoja na ukweli kwamba yalikuwamo mataifa makubwa
na yenye nguvu za kiuchumi kama vile China na Indonesia.
“Alikuwa ni Mwalimu na
Helmut Kohl wa Ujerumani Magharibi wakati huo, waliokuja na wazo la haki sawa
ya kiuchumi kwa wote duniani, hivyo kunzaliwa kwa “International Economic
Order.”
Marekani kinara Tuzo za
Nobeli
Rekodi zinaonyesha kuwa
Marekani ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watu waliopata tuzo nyingi zaidi za
Nobeli, wakifikia watu 334, ikifuatiwa na Uingereza tuzo 117, Ujerumani tuzo
102.
Katika Afrika, mbali ya
Ellen Sirlef wa Liberia aliyechangia tuzo hiyo na mwenzake, Leymah Gbowee,
wengine waliopewa tuzo hizo ni Wangari Maathai wa Kenya, Wole Soyinka wa
Nigeria (katika fasihi mwaka 1986), Kofi Annan wa Ghana (katika amani-2001),
Nelson Mandela na Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini. Misri pia imetwaa tuzo
nne.
Tuesday, October 14, 2014
Nyerere kupata tuzo ya Nobel ya Amani Mwaka 2100
Medali ya tuzo ya Nobel |
Tuzo za Nobel ni maarufu zaidi katika orodha ya tuzo mbalimbali duniani. Tuzo hizo ambazo zilianza kutolewa mwaka 1901, ni matokeo ya wosia alioucha Mswidi Alfred Nobel (1833-1896) mwaka 1895. Alipofariki alikuwa na utajiri mkubwa ambao alipenda uwaendee watu waliotoa mchango katika ujenzi na uboreshaji wa maisha ya binadamu katika dunia yetu.
Tuzo za Nobel zimegawanywa katika makundi sita; watu wenye kutoa mchango uliotukuka kwenye Fizikia, Kemia, Biolojia(Tiba), Riwaya (Uandishi), Uchumi na wale wenye kujishughulisha na masuala ya amani.Tuzo hizi hupewa mtu ama taasisi/ asasi yeyote iliyo/ aliyefanya kazi bora katika moja ya maeneo tajwa hapo juu lakini pia asiyepingana/isiyopingana walau wazi wazi na fikra za kibepari na asionekane tishio kwa mfumo huo wa maisha.
Tuzo hizi wamepokea watu toka takribani mabara yote duniani. Hapa naangazia, japo kwa ufupi tu, tuzo ya amani ya Nobel. Ukitazama orodha ya wapokea tuzo hiyo ya amani utaona wapo waume kwa wake, wenye kujishughulisha na kazi anuwai, watu wa imani tofauti, wazee kwa vijana. Na kijana mdogo zaidi kuliko wote kuwahi kupokea tuzo hiyo ni bi Malala Yousafzai (1997). Binti Yousafzai ameshinda tuzo hiyo pamoja na mwanaharakati mwingine kwa mchango wao katika kutetea/kupigania haki ya elimu kwa vijana.
Litania ya washindi wa tuzo hii ya amani ni ndefu na yenye majina makubwa. Kwa uchache utamkuta Martin Luther King Jr, Mama Tereza wa Kalkuta, Elie Wiesel n.k. Afrika ina uwakilishi mkubwa ambapo nchi ya Afrika Kusini ikiwa imetoa watuzwa wengi zaidi barani humo. Kwa uchache tu kuna Albert Lithuli(1898-1967); mmoja wa marais wa ANC na Mwafrika wa kwanza kupata tuzo hiyo, Nelson Mandela (1918-2013), Desmond Tutu n.k. Afrika Mashariki yupo kwenye orodha hiyo hayati Wangari Maathai (1940-2011 ) mwanamke wa kwanza barani kupokea tuzo hiyo kwa mchango wake kwenye upandaji miti.
Julius Kambarage Nyerere (1922- 1999) kiongozi wa kwanza mzalendo wa Tanganyika huru na baadaye Tanzania, ni mmoja ya viongozi walioshiriki kujenga utu wa mtu duniani. Ushahidi wa mchango wake kutetea utu wa mwanadamu hususani binadamu mwafrika upo wa kutosha. Kwenye imani na kanuni za mwanaTANU, kanuni moja inasema binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja (sisemi kwa mpangilio kama ilivyo). Kiongozi huyu, kupitia sera ya chama na nchi yake, alijitoa kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa huru. Mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi kwa nchi za kusini mwa bara hili la kitropiki, bara lenye kuandamwa na magonjwa ya kila namna ya asili na hata ya majaribio.
Sera za Tanganyika na baadaye Tanzania ziliruhusu wapigania uhuru wa nchi kadhaa za kusini mwa Afrika kuweka makazi yao na kufungua vituo vyao vya mafunzo nchini Tanzania. Mfano ni wapigania uhuru wa Afrika Kusini kule Morogoro, wapigania uhuru wa Msumbiji kule Mtwara na kadhalika. Zaidi wapigania uhuru na haki za watu kadhaa waliifanya Tanzania kuwa nyumbani kwao kwa namna moja ama nyingine ambapo walijipanga na kuweka mikakati ya ukombozi wa nchi zao. Unaweza kuwataja wachache tu hapa Laurent Kabila (1939-2001) wa Kongo-Kinshasa, John Garang (1945-2005) wa Sudan, Yoweri Museveni (1944) wa Uganda
Tanzania kwa miaka mingi imekuwa nyumbani kwa wakimbizi toka nchi mbalimbali zenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.Tanzania na Zambia zinatajwa na mwandishi Crawford Young kwenye kitabu chake cha "The Postcolonial State in Africa: Fifty years of independence. 1960-2010" cha mwaka 2012, kuwa ni mataifa yenye makabila mengi lakini mataifa haya yameendelea kuwa ni nchi zenye amani na demokrasia. Nikiongelea AMANI ya Tanzania, pamoja na kwamba kuna tofauti lukuki kwa wananchi wake katika masuala ya imani, makabila na hivi karibuni itikadi tofauti za kisiasa, ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na viongozi wa mwanzo wa Tanganyika na baadaye Tanzania na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa miongoni mwao. Amani hiyo, pamoja na kuwa zawadi toka kwa Muumba, ilijengewa mazingira ya kustawi na viongozi hao wa mwanzo. Matumizi ya lugha moja - KISWAHILI, kwa taifa kubwa lililokuwa na vitaifa vingi (makabila) kabla na mara baada ya kupata uhuru, ni mbinu na mchango mkubwa uliostawisha na kuendelea kustawisha amani na mshikamano kwa Watanzania na pia kutoa hifadhi kwa binadamu wa mataifa mengine.
Mchango wa Tanzania kumfukuzilia mbali kiongozi wa mabavu wa zamani nchini Uganda Idi Amin Dada ilikuwa mchango mkubwa wa kazi ya amani kwa Tanzania, Uganda, Afrika na duniani kwa ujumla.
Orodha hii inaweza kuwa ndefu zaidi, tukomee hapa kwa leo lakini tujiulize swali kwanini pamoja na mchango mkubwa amabao Tanzania imetoa katika masuala ya amani kwa ustawi wa binadamu nchi hii haijapewa zawadi hiyo na Nobel ya amani. Si kwamba bila tuzo hiyo maisha hayaendi la hasa, hata bila tuzo hiyo tunaendelea kuishi kwa mshikamano na udugu. Twauliza swali hilo kwa kuwa vigezo vinavyotumika kuwapima watu mbalimbali duniani inatakiwa ziwe kwenye mizani iliyo sawa.
Binadamu, kama ilivyo kwa maji huwa ana tabia ya kufuata mkondo katika maamuzi yake. Tanzania, kupitia Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wa zama zake, ilikuwa ikifuata mfumo wa ujamaa na kujitegemea. Mfumo huu si rafiki sana kwa nchi za magharibi na hivyo Norway na hususani wakfu wa Nobel hata kama wanakubaliana na mchango wa Mwalimu Julius Nyerere si rahisi kwao kutaka kujihusisha na nchi ama kiongozi mwenye kujitangaza hadharani kuwa ni mjamaa, mfumo wenye kupingwa kwa nguvu zote na Marekani, Uingereza na jumuiya za kibepari zenye "kuufadhili" wakfu huo.
Mwalimu Julius Nyerere, kwa mtazamo wangu kupitia mchango wake kutetea haki ya wanyonge kwa mfano wake wa kujinyima, anastahili kupata tuzo hiyo ya amani. Tatizo ni kizazi hiki za watoa tuzo hizo na "wafadhili wao" wana upofu kwenye masuala yenye kugusa ujamaa na upofu huo nadhani utakwisha 2099 karne moja baada ya kifo chake. Ila wahenga walinena vyema mno na ni vyema kufuata maelekezo yao: Tenda wema nenda zako...
Martin Mandalu
Alice, 14/10/2014
Martin Mandalu
Alice, 14/10/2014
Saturday, September 20, 2014
Baadhi ya Miamba Afrika
Mwanamuziki Mkongwe wa Kameruni |
Mwanamuzi mashuhuri wa Kongo - Hayati Franco |
Mwanamuziki Mashuhuri wa Nigeria Hayati Fela Kuti |
Mwanamuziki wa Zimbabwe Mashuhuri Oliver Mtukudzi |
Mwanamuziki wa zamani Tanzania Frank Humplick |
Mwanamuziki nguli wa Mali Salif Keita |
Mwanamuziki wa Senegal |
Mwanamuziki Maarufu nchini Tanzania hayati Marijani Rajabu |
Mwanamuziki Mashuhuri nchini Tanzania hayati Mbaraka Mwaruka Mwinshehe |
Saturday, August 30, 2014
NYAMA CHOMA NA UCHUMI WA TANZANIA
PICHA KWA HISANI YA BLOGU WAANDAA TAMASHA |
Nyama
choma ni chakula cha kitamaduni kwa baadhi ya jamii nyingi barani Afrika na
hata duniani. Historia inaonyesha kuwa jamii ama makabila mengi hapo kale
ziliishi/yaliishi kwa uwindaji wa wanyama pori. Hivyo nyama choma imekuwa
ikiliwa toka enzi za kale barani ila katika baadhi ya jamii tu. Jamii nyingine
ziliishi kwa kula mizizi na matunda pori. Wanahistoria wanaweza kutusaidia
katika hili, kuibuka kwa shughuli kuu na maalumu kwa jamii mbalimbali zama za
hivi karibuni ama nyuma kidogo, kulisababishwa na shughuli zale za uwindaji naukusanyaji mizizi na matunda pori.
Baadhi
ya makabila yakawekeza nguvu na muda wao katika uwindaji na baadaye kuwa
wafugaji, na mengine katika ukusanyaji mizizi na matunda pori na kisha kuwa
wakulima.Na kulikuwa na wavuvi halikadhalika na leo waendelea pia. Kwa hivi
basi wawindaji na baadaye wafugaji bila shaka hawa walikuja kuwa wala nyama ila
hali wakusanya mizizi na matunda pori baadaye wakawa wakulima wa mazao mbali
mbali. Mambo haya yalitokea zama za kale za mawe na chuma. Mawe na baadaye
chuma kilikuwa chombo cha kuwindia wanyama na pia zana ya kutifua ardhi na
kulimia mashamba. Hayo yalifanyika enzi hizo; hivi leo mambo haya yamebadilika.
Siku hizi kila mtu anakula nyama na tena kuna matamasha ya nyama choma. Ila
kabla ya matamasha ya nyama choma ya kisasa tuangalie nyama choma za sehemu chache nilizozifahamu miaka ya tisini.
Miaka
hiyo nilikuwa mwanafunzi mkoani Iringa. Nilisafiri kwa treni ya kati toka
Shinyanga, mara nyingine toka Mwanza hadi Dar es Salaam na mara nyingine
nilishukia Dodoma. Toka Dar es Salaam nilipanda basi hadi Iringa, ama nilipanda
treni ya Tazara mpaka Makambako na kisha kwenda mjini Mafinga, ambako palikuwa
nyumbani kwangu kwa miaka mitano. Safari kwa treni ya Tazara ilikuwa ya kitalii
na ya kuvutia, kwani nilipata fursa kuwaona wanyama wengi: swala, twiga, tembo
n.k. Ama niliposhuka Dodoma nilikwenda Iringa kwa njia ya “Ny’ang’oro” barabara
iliyokuwa na kona nyingi za kutisha na tena njia hiyo ilikuwa ni ya hatari,
kwani mara nyingine magogo yaliwekwa njiani na majambazi na kisha abiria
kunyang’anywa mali zao baaada ya basi kusimama. Namshukuru Mungu sikuwahi
kukutana na dhahama hiyo. Njia hii pamoja na kadhia zake ilinifurahisha kwani
nilikuwa na uhakika wa kula samaki watamu pale Mtera. Sijui mambo yanakwendaje
huko siku hizi kwani sijafuatilia taarifa za huko na sijapita huko tena miaka
mingi sasa.
Toka
kanda ya ziwa kwa treni watu wengi tulifurahia ujuzi wa wenyeji wa Saranda wa
kuandaa “nyama choma.” Kile kituo cha treni Saranda wengine hupaita
“Kilimanjaro Hotel”. Kila zama na kitabu
chake, enzi hizo Kilimanjaro Hotel ilikuwa ndiyo Hotel pekee? ya
hadhi ya juu zaidi jijini Dar es Salaam na wageni wengi maarufu walifikia pale.
Saranda, moja ya vituo vya treni ya kati kilichopo mkoani Singida, ni maarufu
mno kwa uuzaji wa kuku wa kienyeji. Hivyo hapo tulikula nyama choma, sikumbuki bei ya kuku wale wasioisha, iwe masika iwe kiangazi
bado utawapata. Bei ya kuku wale abiria wengi daraja la tatu tuliimudu,
sifahamu abiria waliokuwa mabehewa ya daraja la kwanza na la pili kama wao pia
walikula nyama choma ile. Kwa daraja la tatu, sina shaka, naelewa vyema kwani
nilishuhudia abiria wengi wakila “nyama choma” ya Saranda.
Kutoka
Iringa Mjini kwenda Mafinga, unapita maeneo mengi kadhaa moja muhimu huwezi
kulisahau ni Tanangozi; maarufu kwa nyama choma ya aina yake. Hapa sikupata
nafasi ya kula nyama choma ila nafahamu huduma hiyo ilikuwepo. Mjini Dodoma,
kule Mnadani kulikuwa na nyama choma za uhakika, sijui siku hizi, tena bei yake
ilikuwa rafiki kwani wananchi wa kipato cha kawaida waliimudu. Naambiwa baadhi
ya ndugu wabunge walifika kule kupata nyama choma pia. Najua kuna maeneo
mengine mengi yaliyokuwa yakitoa huduma hii kwa wahitaji tena kwa bei
maridhawa.
Ugumu wa maisha kipimo cha akili ama uvumbuzi
mama wa maendeleo, hivi karibuni hususani jijini Dar es Salaam kumeibuka
matamasha ya nyama choma. Kama tulivyoona hapo awali hili si jambo jipya na kuliona
kama uvumbuzi. Upya wa nyama choma hii ni kule “kusasaishwa” ambapo kuna kuwa
na eneo mahususi la kuendesha shughuli hiyo, ndani ya eneo ambamo kuna kuwa na
mambo anuwai yakiendelea ikiwa ni pamoja na ajira kadhaa za muda; mama/baba
lishe, biashara mbalimbali mfano uuzaji vinywaji, na bidhaa nyingine lukuki.
Ili kuingia eneo hilo ni lazima kutoa kiingilio. Nimeona matangazo kiingilio
mara nyingine huwa shilingi za Tanzania elfu saba 7,000/= hadi kumi elfu 10,000/=.
Kiingilio hicho si tiketi ya kwenda kunufaika na kila huduma kwenye tamasha
hilo, muingiaji atalazimika kuendelea kutoa pesa kwaajili ya huduma zingine.
Kwa haraka haraka nyama choma hii si kama ile ya Mnadani ama Saranda, hii ni
kwaajili ya watu wa tabaka maalumu.
Kwa
hakika matamasha ya nyama choma ya namna hii yanawalenga watu wenye ahueni kubwa
ya maisha. Ni jambo jema ama jambo baya si lengo la makala hii leo. Hapa
najiuliza tu je, hizi ni dalili za kukuwa kwa uchumi wa taifa la Tanzania
ambapo wananchi, baadhi yao, wanapata kipato cha matumizi ya ziada, matumizi
yasiyo ya lazima? Sera ya maendeleo ya Taifa inalenga kuwa ifikiapo mwaka 2025
jamii ya Tanzania iwe na watu wenye uchumi wa kati. Hii maana yake Mtanzania
mmoja anakuwa na uwezo wa kutumia kiasi cha dola za Marekani 5,960, yaani pesa
ya Tanzania 9,536,000/= kwa mwaka walau kitakwimu, ama shilingi 26,126/= kwa
siku. Kulingana na ripoti ya maendeleo ya binadamu ya shirika la maendeleo la
Umoja wa Mataifa ya mwaka 2014 Mtanzania wa leo, kitakwimu, ana uwezo wa
kutumia dola za kimarekani 1702, yaani wastani wa pesa ya milioni mbili laki
saba ishirini na tatu elfu na mia mbili 2,723,200/= kwa mwaka, ama wastani wa
shillingi elfu saba na mia nne na sitini 7,460/= kwa siku. Hii ni kama pato
jumla la Taifa litagawanywa kwa kila mmoja wetu. Utagundua kuwa kwa uchumi
tulionao hivi sasa kitakwimu yaani kila Mtanzania kuweka mfukoni mwake shillingi
7,460/= tamasha la nyama choma litakosa wateja. Kwahiyo, ni dhahiri kuwa matamasha
ya nyama choma ni kwaajili ya watu mahususi. Lakini inawezekana pia
kuwa wingi wa matamasha ya nyama choma na maisha ya mtindo huo ni kiashiria cha
kukua kwa tabaka la kati katika uchumi wa Tanzania.
Swali
hapa ni je uchumi wa Tanzania umekuwa kiasi cha kuwa na matamasha ya nyama choma mengi vile, ila hali uwanja wa mpira wa
taifa unaweza kujazwa na watu wenye bahasha za kaki? Je, uchumi wetu umekuwa
kiasi cha kutosheleza sherehe kila uchao wakati imani za kishirikina zimetujaa
mpaka shingoni? Mauji ya albino yanaendelea kila uchao. Je, hii ni jamii ya watu
tusioelimika? Uchumi mkubwa wa wala nyama choma hauwezi kumkata kiungo binadamu
mwenzake kwa kisingizio cha kupata mali. Uchumi uliokuwa na kukomaa watu wake
hufanya kazi halali kwa bidii zaidi, hulipa kodi, huheshimu tofauti zao na watu
wengine katika jamii, hutimiza wajibu wao iwapasavyo na kisha huenda kwenye
TAMASHA LA NYAMA CHOMA.
Tuesday, August 12, 2014
Tukumbushane Upendo na Uzalendo wa Taifa letu
Picha kwa hisani ya blogu ya Ikulu, Dar es Salaam |
Maneno ya Wimbo Wa Taifa wa Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Wabariki viongozi wake
Hekima umoja na amani
Hizi ni ngao zetu
Afrika na watu wake
Ibariki Afrika
Ibariki Afrika
Tubariki watoto wa Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na umoja
Wake kwa waume na watoto
Mungu ibariki
Tanzania na watu wake
Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania
Friday, August 1, 2014
The Continent is not short of Heroes!
Dr. Sheik Umar Khan (1975-2014) - Photo by BBC |
Dr. Matthew Lukwiya (1957-2000) Photo by Wikipedia |
"It is our vocation to save life. It involves risk, but when we serve with love, that is when the risk does not matter so much. When we believe our mission is to save lives, we have got to do our work." Dr. Matthew Lukwiya
Dr. Lukwiya and Dr. Khan died while serving their people-treating patients of the EBOLA disease
This is indeed the spirit of "for my people and my country"- let political leaders in Africa take these two men as models and keep the social contract dear in their hearts as they serve their fellow citizens just like these two scientists.
Saturday, July 26, 2014
SOKO LA KIBEPARI NA PANDE ZAKE MBILI
Wachumi
na wapiga debe wa “mfumo wa uchumi wa soko
wenye ubinadamu” ( The market friendly approach ) [Tafsiri hii ni yangu binafsi
] ambao lengo lao ni kuona uchumi unakuwa, kupitia mabadiliko katika
taasisi, kupunguza rushwa, na kuhakikisha maisha ya watu kupitia huduma muhimu
kama afya, elimu, uhakika wa chakula na kadhalika yanakuwa bora zaidi. Njia hii
ni mbadala wa njia zingine zilizotangualia (sitaki kuingia katika nadharia hii
ya Neo-liberalism kwa ndani).
Nadharia
hii yenye kulenga kupunguza umasikini inazishauri nchi “masikini” kushirikisha Serikali na
sekta ya umma kukuza uchumi na kupambana na umasikini. Kwa hiyo wadau wakubwa
wa kujenga uchumi na kupunguza umasikini katika jamii ni wadau hao wawili;
serikali na sekta binafsi. Nadharia hiyo inashauri uchumi kwa kiasi kikubwa
uendeshwe na sekta binafsi ilhali serikali iandae miundo mbinu na mazingira yenye
kuiwezesha sekta binafsi katika shughuli za kujenga uchumi; lakini serikali
inapewa jukumu na fursa ya kuirekebisha sekta hiyo binafsi yenye jukumu kubwa
la kuzalisha uchumi. Kwahivi serikali kazi yeke kuu ni kusisimua, kuibua fursa,
kujenga mazingira na kurekebisha wazalishaji pale wanapoelekea kupotoka.
Nadharia hii ina mashabiki na pia wapinzani wa kutosha tu:
lengo la makala hii hata hivyo si kuichambua nadharia hii bali kuongelea kwa ufupi tu mfumo
wa biashara nchini Afrika Kusini. Naongea kupitia uzoefu wangu wa miezi
michache nchini Afrika Kusini; nitaandika kwa uhuru kama nilivyokuwa nikifanya
wakati wa kuandika insha shule ya msingi hadi kidato cha kwanza. Tuliandika kwa
uhuru mkubwa na kutumia vizuri zaidi hisia, kumbukumbu na uzoefu wetu. Hatukubanwa
na takwimu, ambazo kwenye makala za baada ya shule ya msingi tumefundishwa kuwa
ni muhimu na mara nyingine lazima. Sasa tuangalie biashara nchini Afrika
kusini.
Afrika Kusini ina mfumo wa kipepari; uchumi wake kwa kiasi
kikubwa unaendeshwa na soko. Natazama hapa soko la mahitaji ya kila siku ya
binadamu. Moja ya sifa ya nchi za kibepari ni kuunganisha bidhaa za mashambani
katika mfumo wa soko wa bidhaa za viwandani. Kwahiyo masoko yanakuwa na bidhaa
za mashambani na viwandani hali kadhalika. Hivyo katika soko moja utakuta viatu, nguo na kadhalika [n.k] (bidhaa za viwandani), nyanya, maboga, mahindi
mabichi, n.k (bidhaa za mashambani). Najua masoko yetu pia yanafanya hivyo ila
kuna tofauti kubwa iliyopo kati ya masoko yetu Tanzania na ya Afrika Kusini [A.K].
Masoko nchini Afrika Kusini ambayo mengi ni mtandao wa
wamiliki kadhaa wenye nguvu ya uchumi yamewekwa katika namna ambayo hupatikana
katika miji karibu yote. Masoko hayo makubwa kwa kawaida hupatikana katika miji
midogo, mikubwa na majiji. Eneo moja huweza kuwa na makampuni kadhaa ya
kibiashara, kulingana na ukubwa wa mji na uchumi wa eneo husika. Kwa Tanzania
mfano sahihi ni ule wa soko la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Soko la Mlimani City, Dar es Salaam |
Kama ilivyo kwa Mlimani City, Dar es Salaam, masoko ya A.K
hujumuisha makampuni kadhaa ndani yake. Muhimu na kubwa zaidi ni kuwa masomo
hayo, kwa kawaida, yameunganishwa na mfumo wa kibenki ambapo wateja wana uhuru
wa kuingia na pesa taslimu ama kadi za benki zenye pesa ndani yake. Mteja huchagua
bidhaa anazotaka na kulipia kwa njia iliyo muafaka kwake; kwa pesa taslimu ama
kwa kuchanja kadi yake ya benki.
Kwa kawaida Masoko hayo huwa na umeme wa uhakika muda wote;
kwa kuwa kuna bidhaa zenye kuhitaji majokofu. Nyama, Samaki, vinywaji
mbalimbali n.k. Lakini pia mfumo wa malipo huhitaji umeme muda wote. Zaidi masoko
haya ni chanzo kikubwa cha ajira; watu wengi hupata fursa za kufanya kazi za
aina mbalimbali. Unaweza kuorodhesha nafasi chache tu hapa: wauzaji (wapokea
pesa), wapanga bidhaa, wakagua bidhaa, wasukuma mikokoteni, n.k
Masoko ya A.K yana sifa nyingine muhimu ya kuwa na wateja
wenye kupenda kufanya manunuzi (nadhani hii ni kutokana na uimara wa
uchumi na aina ya utamaduni); wananchi wengi
wana uwezo kununua bidhaa nyingi na kulipia kila bidhaa walioichagua.
Utakumbuka mfumo wa soko wa aina hii unauza karibu kila kitu kinachohitajika
katika matumizi ya mwanadamu. Wakati sehemu nyingi nchini Tanzania uchumi wetu
unaruhusu mtu kujipatia mahitaji yake toka vyanzo vingine mbali na soko; mfano
kwenye bustani yake atakula machungwa, maembe n.k, toka shambani kwake atakula
viazi, mihogo n.k. Nchni A.K bidhaa nyingi kwa watu wengi hupatikana kwenye
masoko hayo tu.
Ni utamaduni wenye uzuri na ubaya wake pia; si
lengo langu kukugusa mada hii kwa undani hivi leo, lakini inafaa kusema chochote juu yake. Mfumo huu wa soko
una faida lukuki lakini pia mapungufu hayakosekani. Nitaelezea jambo moja tu
kwa kila upande uzuri na udhaifu wake.
Mfumo huu wa soko, ni njia ya uhakika ya ukusanyaji kodi.
Serikali kupitia mamlaka zake husika hukusanya kodi kwa uhakika kabisa. Kodi,
twafahamu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani. Ni kupitia kodi ndio
serikali inapata nguvu ya kuwapatia wananchi wake hudumu za msingi kama
hospitali, shule, n.k
Mfumo huu wa soko, kwa maoni yangu, una shida kwenye bidhaa
za vyakula. Wahitaji wa bidhaa kadhaa mara nyingine ni wengi kuliko uzalishaji
wa asili unavyoweza kumudu mahitaji ya wateja hao. Ili kukidhi mahitaji hayo
basi ni lazima kutafuta njia ya uzalishaji ambayo ni ya bandia, matumizi ya
teknolojia yanaingia hapo. Si kila jambo linalotumia teknolojia ni jema. Chukua
uzalishaji wa mayai kwa njia ya asili. Kwa kawaida kuku anapotaga yai basi kwa
siku ni yai moja tu. Lakini kuna watu wanakula zaidi ya yai moja kwa siku.
Hivyo basi ili kukidhi haja ya walaji lakini na ili kupata faida haraka ni
lazima teknolojia iingie kati na kuzalisha mayai mengi kwa siku moja. Mfano huu
unaweza kutumika kwa bidhaa nyingine za vyakula. Mfumo huu unalzimu bidhaa
nyingi za vyakula kuzalishwa kwa teknolojia. Hivyo bidhaa nyingi za vyakula
zinakosa virutubisho na viini asilia ambavyo sehemu nyingi nchini Tanzania bado
tunaendelea kuvifurahia…
Mambo mengi ndivyo yalivyo, kama sarafu, yana pande mbili…
Baadhi ya makampuni ya kibiashara nchini Afrika Kusini,
ambayo baadhi yake hupatikana pia Afrika Mashariki ni pamoja na Picnpay,
Spar,Checkers, Shoprite, Pep, mrprice, edgers,
kfc, lewis, steers, jetmart
Subscribe to:
Posts (Atom)