Na. Theddy Matemu Sawaki
Fursa zipo kila sehemu - This image for education purpose is taken from another website |
Tofauti na
elimu ya darasani lakini mambo ya elimu dunia Zingatia yafuatayo.
Ø Kujali muda.
Ø Kuheshimu kila mtu.
Ø Kujituma.
Ø Kujifunza lugha na tamaduni
za wenyeji.
Ø Kuwa msikilizaji zaidi
ya msemaji.
Ø Kuwa tayari kupokea
ushauri toka kwa watu wote hata wa kada za chini.
Nimekuwa nikizunguka kwenye mitaa ya Mji wa
Tokyo nikaja kugundua wahindi ni watu wanaojua kucheza na fursa wanazozipata.
Sio kwa nchi zinazoendelea tu hata kwa nchi zilizoendelea kama Japani.
Na
nikaamini kuwa darasani tu haitoshi kukufanya ukapata maendeleo ya Kimaisha.
Kwa kuwa napenda kula nimekuwa nikizunguka katika mitaa ya Tokyo kutafuta
chakula ninachokipenda. Nimekutana na migahawa ya Kijapani na kihindi na
kitaliano.Migahawa ya kihindi ina sehemu ndogo sana ya kufanyia biashara
naamnisha ukubwa wa nyumba maana jiko liko hapo hapo na viti vya kulia wateja
viko hapo hapo karibu( ila kwa huku wamejitahidi kwa usafi sio kama
wanavyoutufanyia kwetu Tanzania)hapo napo ni kipengele kingine
cha kujifunza kumbe kuwa wasafi wanaweza isipokuwa ni namna gani nchi husika
inajali wananchi wake.
Katika
kufanya utafiti wangu wa kichumi usio rasmi (mimi sio mwana uchumi) nikagundua
wahindi wameweza kujenga umaarufu katika biashara ya chakula na wana wateja
wengi sana wenyeji wa Japani. Nikamwuliza mmoja wa wenye migahawa wa kihindi
umewezaje kufanikiwa katika kupata wateja wengi akaniambia nina miaka 30 hapa Japani
na kweli anaongea kiJapani kama amezaliwa nacho.
Kwanza
kabisa alipofika hapa alijifunza lugha (naweza sema kwa Japani ili uweze kuishi
vizuri ni vyema ujue lugha vinginevyo utapata shida katika huduma za muhimu),pia
alijifunza tamaduni na mengine muhimu katika maisha ya waJapani. Hii ilimsaidia
kuweza kuwasiliana na wateja wake, kujua nini wanapenda na nini hawapendi kujua
jinsi gani angeweza kuwafanya wafurahie huduma zake. Haya yote alifanikiwa pale
alipoajiri wafanyakazi wa kijapani wakati akianza biashara yake na kuwafundisha
jinsi ya kuandaa vyakula vya kihindi nao wakamfundisha lugha na mengine yote ya
muhimu.
Alipoona
biashara imeshamiri alipunguza wafanyakazi wake. Baada yakupunguza wafanya kazi
biashara ikayumba sana. Akaitisha kikao na wafanya kazi wake waliobaki kutaka
kujua tatizo ni nini kama unavyojua wafanyabiashara wengi wa kihindi hupenda
kuamrisha zaidi na huamini watu wachache tu.
Mmoja
wa wafanyakazi akamwambia bosi ili biashara ikue warudishe wale wafanyakazi
uliowapunguza kwasababu wanajua siri ya kazi na wameizoea na ndio walichangia
biahara kukua. Hapo ndipo alipojifunza kwamba ili upate mafanikio lazima uamini
kwamba kila mtu hata kama ni mdogo kiasi gani anaweza kuwa na mchango katika
maisha yako. Muda mfupi baada ya wale wafanyakazi kurudishwa kazini biashara
ikainuka mpaka leo na wateja wanajaa mpaka wanasubiria nafasi ya kuketi kwa
foleni.
Nimejifunza
Maisha sio kukaa darasani tu bali pia na hasa namna gani unaweza kuthubutu na
kufanya chochote hata kama ni nje na nchi yako na ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa
sana, ili mradi kuwe na amani na utulivu katika nchi husika.
No comments:
Post a Comment