Monday, May 13, 2013
KAZI NI MOJA TU SASA
Wanazuoni wa mwaka wa tatu chuoni STEMMUCO kwa juma la pili sasa wamekuwa wakitetea tafiti zao walizofanya kwa mieza kadhaa. Tafiti hizo, ambazo ni sehemu ya wajibu wao ili kupata sifa ya kupata shahada yao ya kwanza, (degree ya kwanza) zilikuwa na mada tofauti tofauti kama jinsi walivyo watu na miguso yao.
Baadhi ya kazi zilihusu mchango wa Chuo Kikuu cha STEMMUCO kwa maisha ya watu wa Mtwara kwa ujumla wake, zingine na nyingi hasa zilihusu masuala kadhaa ya elimu. Kwanini shule za Mtwara ubora wake wa elimu ni hafifu, kwanini shule za serikali ubora wake mbele ya zile za binafsi ni dhaifu n.k. Zingine zilihusu shughuli za kiuchumi mkoani Mtwara; uzalishaji chumvi na athari zake, mchango wa bandari Mtwara kwa wananchi. Kazi za wanazuoni wengine zilitazama masuala ya kijamii; kuongezeka kwa watoto wa mitaani, Unyago, jando na faida, hasara na changamoto zake. Mazingira pia hayakuachwa nyuma; tafiti kadhaa zimegusia suala hilo. Uhalifu ni moja ya mada zilizojadiliwa hali kadhalika.
Zoezi hili lilifanywa kwa lugha ya kiigereza; vijana wengi walijipanga na kutafuta misamiati stahiki kuelezea kazi zao; wapo waliofanya vyema sana, waliojitahidi sana na wanaohitaji kuongeza bidii zaidi. Kwa ujumla wanazuoni hawa ni hazina kubwa kwa taifa na wito kwao ni kuendelea na moyo wa kitafiti ili kuvumbua vyanzo vya matatizo na kuyafanyia kazi.
Saturday, April 27, 2013
SIKU YA MUUNGANO STEMMUCO
Viongozi waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwl. Julius Nyerere na Mzee Abeid Karume wakitia saini makubaliano Picha kwa hisani ya blogu ya Michuzi |
Mwalimu Julius K. Nyerere akichanganya udogo wa Tanganyika na Zanzibar ishara ya muungano huo. Hii kwa hakika ishara yenye nguvu sana. Picha kwa hisani ya blogu ya Michuzi |
Muungano pamoja na malengo mengine, kwa vyoyote vile ulikuwa na lengo la kufikia maendeleo ya binadamu; maendeleo ya kweli ya Mtanzania na kutoa mfano halisi wa Umoja ama muungano wa bara Afrika.
Mada zilizotolewa pale STEMMUCO zilikuwa pamoja na Muungano na MKUKUTA, Muungano na Uzalendo, Mali asili na Muungano Afrika Mashariki
Friday, February 8, 2013
MITIHANI INAENDELEA STEMMUCO
WATAALAMU WA BAADAYE WAKIONYESHA UJUZI WA MAJUMA 16 KATIKA SAA TATU |
WANACHUO STEMMUCO WAKIENDELEA NA MITIHANI MJINI MTWARA |
WALIMU WAJIPIMA UJUZI WAO KABLA YA KWENDA KUFUNZA WENGINE - MITIHANI |
Subscribe to:
Posts (Atom)