Nchi ya Tanzania, inaendelea na mchakato wake wa kuandika katiba mpya yenye mguso wa moja kwa moja toka kwa WaTanzania walio wengi. Katika juhudi hizo wadau mabalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi, watu binafsi na kadhalika wanafanya juhudi kuwaelimisha wananchi walio wengi na wasio na ujuzi na uelewa wa katiba inayotumika nchini hivi sasa. STEMMUCO kwa nafasi yake imefanya kazi hiyo ya kuwaelimisha wanachuo juu ya katiba inayoiongoza Tanzania kwa sasa. Idara ya sheria, chuoni hapo imeongoza mhadhara wa wazi kwa wote waliopenda ili kuielezea katiba hiyo.
Monday, October 29, 2012
Thursday, October 25, 2012
MCHWA NA MAENDELEO MTWARA
Nguzo yenye kusambaza nishati ya umeme ikisaidiwa kazi hiyo na mti jirani |
Mchwa ni moja ya utajiri mkubwa wa Mtwara, wataalamu wa masuala ya viumbe hai tunawaomba wafanye tafiti zinazowalenga mchwa kuona ni namna gani Mtwara -Mikindani na taifa kwa ujumla linaweza kunufaika na viumbe hawa. Wapo karibu kila sehemu na hushamiri zaidi kipindi cha ukame, huvamia karibu kila kitu kikavu kilicho mbele yao.
Sehemu ya nguzo iliyooza kwa karibu inavyoonekana |
Hii nd'o nguzo iliyooza vibaya kwenye picha ndogo hapo juu |
Katika pitapita zangu nimekuta mji kati kabisa wakiwa wamekula nguzo zisambazazo nishati ya umeme na sikuona juhudi za maana zikichukuliwa kunusuru linaweza kuwa tishio la maisha mjini humo.
Thursday, September 27, 2012
SIKU YA UTALII TANZANIA NA DUNIANI
Kazi ya Sanaa Mji mkongwe MIKINDANI |
Wanayama wakivuka mto huko Serengeti - Tanzania |
Leo ni siku ya UTALII TANZANIA NA DUNIANI: Utalii ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya uchumi duniani. Kuna nchi kadhaa ambazo hutegemea tu uchumi kujiendesha na kuendelea kuwepo. Kikubwa ni uwekezaji wa makusudi na lazima katika sekta hiyo yenye uwezo wa kuzalisha ajira lukuki. Tanzania ina mali asili nyingi mno ambazo ni vivutio tosha vya utalii; moja ya mambo yanayoturudisha nyuma katika hili ni uwekezaji hafifu kwa watu wetu.
Sanaa MIKINDANI - MTWARA
|
Faru weusi huko Ngorongoro - Tanzania |
Leo ni siku ya UTALII TANZANIA NA DUNIANI: Utalii ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya uchumi duniani. Kuna nchi kadhaa ambazo hutegemea tu uchumi kujiendesha na kuendelea kuwepo. Kikubwa ni uwekezaji wa makusudi na lazima katika sekta hiyo yenye uwezo wa kuzalisha ajira lukuki. Tanzania ina mali asili nyingi mno ambazo ni vivutio tosha vya utalii; moja ya mambo yanayoturudisha nyuma katika hili ni uwekezaji hafifu kwa watu wetu.
Uwekezaji huu utazame kwa makini hasa aina ya elimu tuitoayo kwa wanafunzi wetu; kwa kuwa tuna vivutio vingi vya utalii basi tuwe na mitaala yenye kulenga utalii toka shule ya msingi. Shule zetu ziwe na michepuo yenye kuendana na mahitaji ya karne ya ishirini na moja. Kuwe na shule zenye kuangazia masomo ya sayansi na teknolojia yenye kujibu mahitaji ya moja kwa moja ya watu wetu. Tukirudi kwenye utaliii, shule na mitaala yenye kufunza huo utalii zianze mapema kufunza yaliyo ya lazima; uaminifu, ukarimu, lugha za kigeni, na mengine muhimu hiyo itasaidia kutumia vyema rasilimali na utajiri mkubwa tuliopatiwa na Mwenyezi Mungu, kinyume na hivyo tutaendelea kuwalaumu majirani waliojipanga kunufaisha jamii zao na hiyo nd'o hasa jukumu la serikali.
Friday, September 21, 2012
Mashindano ya Hisabati, kemia, Fizikia, Jiografia n.k
Msaani Akitoa burudani kwa umma- Mashindano ya mavazi, mavazi sahihi- picha kwa hisani ya google? |
Nchini Tanzania, nchi yangu hii, kwa maoni yangu naona elimu hatuipatii fursa ya kutosha; ni kweli Serikali na wadau wengine wengi wanajitahidi kwa kiasi kikubwa kutoa huduma hiyo muhimu kwa jamii. Hata hivyo juhudi mara dufu bado yahitajika. Kuna njia na mbinu nyingi elimu inaweza kuiga toka kwenye kada nyingine hapa nchini.
Kwenye Muziki, filamu na sekta nyingine, wadau kadhaa wameanzisha tamasha maalumu kutafuta vijana wenye vipaji, na tamasha hizo zinafanywa kwa mbwembwe,ubunifu na bila shaka udhamini mkubwa na wenye gharama kubwa tu. Jambo hili ni jema sana kwani shughuli hizi zinachangia kuwakwamua vijana toka kwenye kukosa ajira na kuweza kupata kipato ambacho bila shughuli hizo wasingekipata. Hata hivyo wazo na wito wangu: kuibuke wadau wengine watakao fanya mashindano ya vijana kwenye hisabati, fizikia, baiolojia, jiografia, kiswahili... wazunguke mkoa mmoja hadi mwingine kupata wataalamu wa hisabati, na kadhalika. Kufanya hivyo kutatuwezesha kupata teknolojia na kujenga hamu ya kubobea na kujikita zaidi katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Monday, August 27, 2012
Wasanii watakiwa kujiendeleza kitaaluma
Na Mwandishi BASATA
Mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa Filamu Ngalimecha
Ngahyoma akizumza jambo na wadau wa sanaa
ukumbi wa Basata
|
Wasanii wa nchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze kufanya kazi zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchini.
Akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu hapa nchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi katika uandaaji wa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii kutokuelewa misingi ya uandaaji wa filamu.
“Kuna maeneo ya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa utimilifu, na hakuna njia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana lazima mtu ufundishwe. Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini matokeo ya kufanya mambo kwa vipaji ndiyo haya ambayo yanatupa filamu zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,” alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)