Mmoja wa mitaa ya mji wa Mtwara ukiwa ndani ya giza licha ya umeme wa uhakika mkoani humo- mipango miji wako wapi? |
Mkoa wa Mtwara ni moja kati ya mikoa michache nchini Tanzania isiyofahamu kadhia ya mgawo wa umeme. Mkoa haujaunganishwa kwenye mfumo mmoja wa taifa, hapa ni kwa faida ya wakazi wa Mtwara. Kwani hakuna maana kuwa chanzo cha umeme na usiupate umeme huo. Kwa Mtwara ni tofauti na maeneo yenye utajiri mkubwa ilihali watu wake hohehahe wa kutupwa.
Mkoani Mtwara kuna umeme utokanao na gesi asilia; gesi hii asilia inapatikana mkoni humu na hii inajidhihirisha kwa wakazi wa mkoani humo kwani hakuna mgao. Nafahamu kuwa hii ni hali ambayo wakazi wa mikoa mingi wangependa kuiishi. Na katika hali ya kawaida, ungetarajia kukutana na mitaa yenye kumulikwa vyema na taa nzuri za barabarani nyakati za usiku, lakini hali si hiyo. Nyakati za usiku mjini Mtwara kuna giza kubwa sawa sawa na mikoa yenye mgao wa nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya binadamu. Wazo kwa wahusika wakuu hususani wapanga maendeleo ya mji, wajipange na kuweka taa za barabarani katika mitaa ya mji huo wa kusini mwa nchi yetu ili kuupendezesha mji huo, kuongeza usalama wa mji na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi mjini humo.
No comments:
Post a Comment