Saturday, July 16, 2011

Uhuru wa wahadhiri kimawazo

Makala ya Profesa Mbele juu ya uhuru wa kimawazo wa wahadhiri, kwa hakika, imenitia hamu kubwa kuendelea kuijadili. Nadhani ni suala la msingi kabisa kulitazama hasa hivi leo ambapo kuna vyuo vikuu lukuki hapa nchini. Ni muhimu kuupongeza uongozi wa nchi kwa kuruhusu kuanzishwa kwa vyuo vikuu vingi hapa nchini. Vyuo vikuu vingi moja kwa moja vinamaanisha kukua kwa wigo wa fikra nchini. Kuongezeka kwa fikra ni mwanzo wa ugunduzi na kichocheo kikuu cha maendeleo.

Moja ya masuala makuu katika kipindi cha " Scholarsticism" karne ya 12 na 13 ilikuwa ni kuibuka kwa wingi kwa vyuo vikuu vilivyotoa maarifa ya aina mbalimbali. Kipindi hicho Kanisa lilikuwa na mamlaka makubwa hata juu ya kilichofunzwa vyuo vikuu. Matokeo yake kazi za mwanafalsa Aristotle (384—322 BCE) zilikataliwa, hata hivyo kukataliwa huko kulikuwa kwa muda mfupi tu kwani baadaye kazi za gwiji huyo zilianza kufundishwa katika vyuo vikuu na kuboresha zaidi mawazo kwa wanavyuo na wanazuoni.

Kwahiyo basi ni vyema kwa viongozi wa nchi yetu kulitambua hilo na kuwaacha huru wahadhiri wafanye kazi yao, ambayo kimsingi hulenga kujenga wananchi wenye ukomavu wa kujenga hoja na kuzisimamia ili kuendeleza nchi yao na dunia kwa ujumla.

Kupata mawazo zaidi ya Profesa Mbele soma makala hiyo murua kabisa hapa








.

1 comment:

  1. Sikuwa nimeiona hii, kwa vile sikuwa naifahamu blogu hii. Lakini leo nimeigundua hii blogu, na nitaiunganisha kwenye blogu yangu.


    Shukrani kwa kusaidia kusambaza ujumbe wangu kuhusu wajibu na uhuru wa kitaaluma katika vyuo vikuu.

    ReplyDelete