Ni kitabu mahususi kwa kutoa msaada
na mwongozo wa namna ya kumwambudu Yesu Kristo wa Ekaristi Takatifu.
Kitabu hiki kinamlenga kila mwamini
anayemtambua na kumwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu, Mwokozi wa maisha
yake, na nafsi ya pili ya Mungu. Kwahiyo basi, kinawalenga watu wa marika yote;
watoto, vijana, watu wa makamo na wazee.
Kuna jumla ya tafakari 40 ambazo
zote kila moja kwa namna yake zinaongelea maisha ya Yesu katika mahusiano na
wanadamu na baba yake, ambaye ni baba yetu pia. Kitabuni kuna virutubisho vya
kiroho vya kila namna, japokuwa msisitizo ukiwa ni juu ya kumwabudu Yesu
Kristo.
Kitabu hiki kiliandikwa na Dominique Nothomb
(22 Juni 1924 - 9 Novemba 2008) Padre wa shirika la Wamisionari wa Afrika
(White Fathers - M.Afr). Na tafsiri ilifanywa na Martin Mandalu
Mlei wa Jimbo Katoliki Mtwara.
Kitaanza kupatikana hiki karibuni katika maduka ya vitabu. Unaweza kupata nakala yako pia kwa kuwasiliana nami kwa nambari +255767864379 ama +255715864379