Saturday, January 25, 2014

MASOKO YETU NA USAFI


Picha hii inaashiria mambo mengi na moja kati ya hayo ni uchafu. Hii ni sehemu rasmi ya kuhifadhia uchafu karibu na soko kuu mjini Mtwara. Sokoni, kama inavyofahamika, ni sehemu muhimu kwa binadamu kujipatia mahitaji yake muhimu. Soko kwa hakika ni eneo la lazima sana kwa maisha ya binadamu. Pamoja na shughuli zingine muhimu kwa mwanadamu; kula (chakula) ni moja kati ya shughuli za muhimu mno kwa binadamu. Katika hali ya kawaida binadamu ana hitaji kupata chakula kila uchao.

Chakula cha binadamu, hususani mijini, hupatikana sokoni. Kwa Mtwara hupatikana karibu kabisa na jaa hili kubwa la taka.Chakula huingia mwilini mwa binadamu na kuleta manufaa makubwa. Ili chakula kilete manufaa ni lazima kiwe katika hali ya usafi, vinginevyo kitaleta madhara makubwa kwa kiumbe huyu mwenye uwezo mkubwa wa fikra na mawazo mapya. Kwanini binadamu huyu, hususani wa Mtwara asitafute mawazo mapya ya namna kuhifadhi taka mbali na mahali pa kupata mahitaji yake ya kila siku?

Je, ni Mtwara tu ndo jaa la taka li karibu vile na soko? Nini kifanyike? Wataalamu wa mazingira, miji safi, mipango miji n.k watupatie mwongozo...


Monday, January 20, 2014

TAFSIRI PICHANI...


Kitenge (GARY CAMERON_Newscom_RTR)
Picha hii ni kwa hisani ya GARY CAMERON- Newscon-RTR

Picha hii juu inawakilisha ukarimu wa Kiafrika, na hapa hasa, Kitanzania. Tukio hili lilikuwa ujio wa rais wa Marekani huko Afrika Mashariki na hususani nchini Tanzania.

Picha hii inaweza kuwa na malengo kadhaa. Mosi na lililo kubwa kabisa ni ukaribisho kwa rais Barack Obama na familia yake nchini Tanzania. Pili ni ustadi wa matumizi ya tamaduni, hapa kanga na kuwakilisha ujumbe na mchango wa kiteknolojia mahalia kwa dunia. Tatu Afya za Watanzania; ukitazama sawa sawa; utaona kuwa waliovalia kanga hizi ni kina mama wenye afaya njema. Picha hii inaweza kupotosha juu ya afya za watanzania. Kwa uhalisia Watanzania wengi, hususani kule vijijini, hawana afya inayowakilishwa na kina mama hawa wachache wa Dar es Salaam.  Nne ni tabia ya uchafu na ama uchafuzi wa mazingira; utaona kina mama waliopendeza vilivyo ili hali hapo chini wametupa hovyo vyupa vya maji; bila shaka kwa kisingizio kuwa vyupa hivyo vitaokotwa na wahitaji kwa kuwa zahitajika sana siku hizi. 

Msomaji unaweza kutoa tafsiri nyingine nyingi...


Thursday, January 2, 2014

JUA LA MWANZO KABISA TAZANIA 01/01/2014

Jua la Mwanzo wa mwaka 01/01/2014

Mkoa wa Mtwara unapatikana Kusini-Mashariki mwa Tanzania. Pamoja na Kilimanjaro ni mkoa mdogo kabisa kwa eneo. Mkoa huu unapatikana kusini-mashariki kabisa mwa Tanzania, kwahiyo jua nchini Tanzania, huanza kuonekana mkoani Mtwara. Hivyo picha hii japokuwa haina mwonekano mzuri sana, inaonyesha jua la mwanzo kabisa nchini Tanzania siku ya 01/01/2014

MTWARA MITAANI MWISHO WA MWAKA KAZI MTINDO MMOJA

Hata tarehe ya mwisho kabisa ya mwaka watu walikuwa wakiendelea na kazi
Kazi zikiendelea siku ya mwisho wa mwaka kama kawaida 31/12/2013