Monday, October 29, 2012

Mhadhara wa Katiba CHUONI STEMMUCO

Nchi ya Tanzania,  inaendelea na mchakato wake wa kuandika katiba mpya yenye mguso wa moja kwa moja toka kwa WaTanzania walio wengi. Katika juhudi hizo wadau mabalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi, watu binafsi na kadhalika wanafanya juhudi kuwaelimisha wananchi walio wengi na wasio na ujuzi na uelewa wa katiba inayotumika nchini hivi sasa. STEMMUCO kwa nafasi yake imefanya kazi hiyo ya kuwaelimisha wanachuo juu ya katiba inayoiongoza Tanzania kwa sasa. Idara ya sheria, chuoni hapo imeongoza mhadhara wa wazi kwa wote waliopenda ili kuielezea katiba hiyo.








Thursday, October 25, 2012

MCHWA NA MAENDELEO MTWARA

Nguzo yenye kusambaza nishati ya umeme ikisaidiwa kazi hiyo na mti jirani
Manispaa ya Mtwara - Mikindani ina utajiri mkubwa wa kila namna. Kwa uchache utajiri huo unajumuisha, ujuzi wa uchongaji vinyago, ngoma za aina yake, mazao ya kibiashara; korosho, karanga na kadhalika, mali asili lukuki, kina bandari asilia, gesia asilia na kadhalika na kadhalika.





Mchwa ni moja ya utajiri mkubwa wa Mtwara, wataalamu wa masuala ya viumbe hai tunawaomba wafanye tafiti zinazowalenga mchwa kuona ni namna gani Mtwara -Mikindani na taifa kwa ujumla linaweza kunufaika na viumbe hawa. Wapo karibu kila sehemu na hushamiri zaidi kipindi cha ukame, huvamia karibu kila kitu kikavu kilicho mbele yao.





Sehemu ya nguzo iliyooza kwa karibu inavyoonekana


Hii nd'o nguzo iliyooza vibaya kwenye picha ndogo hapo juu

Katika pitapita zangu nimekuta mji kati kabisa wakiwa wamekula nguzo zisambazazo nishati ya umeme na sikuona juhudi za maana zikichukuliwa kunusuru linaweza kuwa tishio la maisha mjini humo.