Friday, March 11, 2016

UBUNIFU KATIKA UCHEKESHAJI?

Ukosefu wa ajira unawafanya vijana kutazama vipaji vyao ili kujipatia kipato na kuendesha maisha yao. Vipaji ni muhimu mno katika furaha ya kweli na utimizaji wa ndoto maishani. Mifumo ya elimu yetu na malezi nyumbani vinapaswa kugundua vipaji vya vijana wangali wadogo na kuwaelekeza huko ili kwamba hata masomo yao yaendane na vipaji hivyo.

Mifumo yetu ya elimu ikifuata ugunduzi wa vipaji vya vijana wetu nadhani, kwa kiasi kikubwa tutaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa sana ukosefu wa ajira. Inawezekana kwa kuwa kila mmoja wetu ana vipaji na uwezo ambao ukinguduliwa na kuendelezwa vizuri atakuwa mtaalaamu kupindukia katika eneo husika.

PICHA KWA MSAADA WA MTANDAO