Friday, June 22, 2012

Nafasi ya Masomo ya juu zaidi



Wanachuo wakifanya mitihani yao Picha kwa Hisani ya wadau wa blogu
Wanavyuo katika vyuo kadhaa nchini Tanzania hivi sasa wanaendelea na mitihani yao ya mwisho wa mwaka.

Tunawatakia mafanikio katika mitihani yao. Mitihani kwa maoni yangu si kipimo bora zaidi kuliko vipimo vingine, ila ndo kipimo cha uelewa kinachokubalika, inawezekana kabisa kukawa na njia nyingine bora zaidi lakini bora hazijakubalika.

Kwa kuwa mitihani ndo njia inayokubalika kupima uwezo wetu basi tuiheshimu na kuifanya kwa bidii na maarifa. Bidii na maarifa vinatakiwa kuja wakati wa maandalizi ili kuweza kumudu na kutawala somo kabla ya kuingia chumba cha mitihani. Ni m uhimu kufanya hivyo ili kujiamini katika kufanya mitihani, kuthibitisha utu na maadili yetu. Ni vyema mtu akafanya mitihani yeye mwenyewe bila kutumia vyanzo visivyoruhusiwa. Kufanya hivyo ni kipimo cha utu bora na faida kwa taifa na dunia kwa ujumla, kwani viongozi na watu wema wamo miongoni mwa wanavyuo wanaoendelea na mitihani yao hivi sasa.

Ili kujijenga zaidi kitaaluma nhapa chini kuna nafasi ya masomo ya uzamili kwa wanaopenda ila nafasi ijazwe haraka kwa kuwa muda umekwisha. Fanya haraka kupata nafasi hii:

 
MASTERS STUDIES - MPhil in African Studies
Our aim is to offer students a window into the cultural, intellectual, and political dynamism of African societies. At a time when Africa is often represented a place in need of outsiders' benevolence and direction, we hope to give students the linguistic and interpretive tools to study African societies on their own terms. The degree will provide an excellent foundation for those who wish to expand their knowledge of Africa, and particularly for students entering positions in the arts, the media, NGOs, and other professions.

The application deadline for MPhil in African Studies 2012-13 is the 30 June 2012

KWA TAARIFA ZAIDI SOMA HAPA

Tuesday, June 19, 2012

BASATA, GABA ARTS WAENDESHA SEMINA KWA WASANII WA FILAMU

Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa asasi ya Gaba Arts James Gayo
akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo kwa wasanii wa filamu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na asasi ya Gaba Arts mapema wiki hii wameendesha semina fupi kwa Wasanii wa filamu ili kuwajengea weledi katika eneo la uandishi bora wa miswada ya sinema (script writing).

Semina hiyo iliyoendeshwa kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa kwenye Ukumbi wa BASATA ilijikita katika maeneo ya namna ya kuendeleza wazo hadi sinema ya kusisimua, namna ya kufikia hisia za watazamaji,ujenzi mzuri wa matukio,kutengeneza wahusika na mfumo wa hadithi, Mwanzo, kati na hitimisho.

Akitoa mada kwenye programu hiyo maalum, Mkurugenzi wa asasi ya Gaba Arts James Gayo alisema kuwa, muda umefika sasa kwa wasanii wa filamu kusaka maarifa ili kutengeneza sinema zenye visa vipya, zenye weledi na zisizosukumwa na matakwa au maelekezo ya wasambazaji.

“Wenzetu kutoka nje wanatamani sana kupata vitu kutoka Afrika vyenye kuzungumza uhalisia wa maisha ya kwetu, wanataka kuona vitu vipya hivyo, katika uandishi wa muswada wa sinema suala la uhalisia na visa vyenye utofauti ni la msingi sana” alisisitiza Gayo.

Alizidi kueleza kuwa watazamaji wa sinema (filamu) huwa wana kawaida ya kuchoka pale wanapolishwa visa vya aina moja muda wote na akaonya kuwa kama wasanii hawatajikita katika kubuni visa vipya na vyenye kugusa uhalisia wa maisha yao wadau watasusia kununua.

“Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi, zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu watatuchoka na baadaye soko litakufa” alionya Gayo.

Gayo ambaye amepitia mafunzo ya utengenezaji filamu katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani alitaja sifa za muswada (script) bora kuwa ni pamoja na kubeba wazo linalozalika kwenye jamii, visa vyenye uhalisia na vipya, utengenezaji mzuri wa wahusika na sifa zingine nyingi.

Kwa upande wake msanii wa mashairi Mrisho Mpoto ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria semina hiyo alisema kuwa, wasanii wa filamu wanahitaji kusaidiwa kwani kwa sasa soko la filamu limekuwa la kitumwa na lenye kuburuzwa na matakwa ya wasambazaji bila weledi.

Akihitimisha programu hiyo, Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego alishauri wasanii wa filamu kujipanga kushirikiana na wasomi wenye weledi katika maeneo yao ili kuzalisha kazi zenye weledi la ubora.

“Tuna wataalam wengi katika Sanaa, wamebanana na mambo mengi lakini ni vema wasanii tukawatumia na kushirikiana nao katika kuboresha kazi zetu” alisisitiza Materego.

Friday, June 15, 2012

FURSA YA WASANII KUJIFUNZA JINSI YA KUANDAA SCRIPT MAKINI KATIKA FILAMU


Ndugu mdau wa Sanaa,
Wadau wa Sanaa wanataalifiwa kuwa Gaba Art Centre wataendesha warsha ya masaa mawili kuhusu Stadi za uandishi wa miswada ya Sinema ( Script writing skills), Siku ya Jumatatu 18,June 2012, saa 4 kamili kwenye jukwaa la sanaa katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni;

1. Namna ya kuendeleza wazo hadi sinema ya kusisimua (Idea to a good film)

2. Namna ya kufikia hisia za watazamaji (Reaching Audience emotion)

3. Ujenzi wa Action na Dialogue nzuri.

3. Kutengeneza Wahusika (Characters)

4. Mfumo wa hadithi, Mwanzo, kati na Hitimisho ( Ploting, beginning, middle and end)

Ni fursa nzuri kwa Wasanii kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya filamu kwani kumekuwa na changamoto mbalimbali katika tasnia hii ambazo kwa njia moja au nyingine zimekuwa kikwazo katika kufikia ufanisi unaohitajika

Mbali ya kukualika wewe binafsi, ninakuomba uwaalike wanachama wako wote wanaoweza kunufaika na mafunzo haya.

KARIBUNI SANA

James Gayo (coordinator)

+255270006

Monday, June 11, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


National Arts Council BASATA

FURSA YA WASANII WA TANZANIA KUSHINDA EURO 5,000 KATIKA SHINDANO LA KUTUNGA WIMBO RASMI WA KUNDI LA MATAIFA YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI

(ACP GROUP OF STATES)

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo limepokea mwaliko wa Wasanii wa Tanzania kujitokeza kushiriki shindano la kutunga wimbo utakaokuwa unatumiwa kama wimbo rasmi wa mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP Group of States).

Shindano hili ambalo litahusisha mataifa 79 wanachama wa umoja huu limeandaliwa na Sekretarieti ya ACP kwa lengo la kupata wimbo ambao utabeba dhana ya mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya ACP, shindano hili linamhusu msanii mmoja-mmoja au Kikundi cha wasanii ambao watapaswa kutunga wimbo huo kwa kuzingatia lengo kuu la umoja huo ambalo ni Maendeleo Endelevu na Upunguzaji Umaskini sambamba na Ushawishi mkubwa kwenye Uchumi wa Dunia.

Aidha, wimbo huo utatakiwa uwe wenye kujenga moyo, fikra na kutangaza malengo ya kundi hili la mataifa ya Afrika, Pasifiki na Karibiani.

BASATA inatoa wito kwa wasanii wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hili kwani ni heshima na fursa pekee tumepewa kama taifa kuonesha vipaji na uwezo wetu kimataifa katika eneo la utunzi wa nyimbo.

Ni wazi kuwa, kujitokeza kwa wasanii wetu wengi kushiriki katika shindano hili si tu kutaonesha utayari wa sisi kama taifa katika kushindana na mataifa mengine wanachama bali utakuwa ni mwanya wa kuitangaza Sanaa yetu ya muziki nje ya mipaka yetu.

Ikumbukwe kuwa, ushindi wa Msanii kutoka Tanzania kwenye shindano hili kutamjengea heshima msanii husika na taifa kwa ujumla.

Maelekezo kuhusu Wimbo utakaotungwa

• Tungo zote lazima ziandikwe katika moja ya lugha rasmi za ACP ambazo ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniyola na Kireno.

• Wimbo huo uliokamilika lazima uambatanishwe na tunzi (lyrics) zilizoandikwa na zitumwe katika mfumo wa MP3/DVD/WAV Format

• Tungo ziguse maeneo yafuatayo

i) Fikra ya umoja ambayo itaunganisha nchi wanachama wa ACP

ii) Utajiri na tamaduni mbalimbali zilizo katika nchi wanachama wa ACP

iii) Mataifa wanachama wa ACP na kuheshimu Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora.

iv) Nchi wanachama wa ACP na msisitizo katika maendeleo yenye usawa pia kusimamia mikataba ya kimataifa ya Haki na Amani.

Jinsi ya Kushiriki

Nyimbo zilizotungwa kwa kufuata mwongozo huo wa ACP zitumwe kupitia anuani ifuatayo ;-

Josephine Latu-Sanft (Press Office)

Avenue Georges Henri

451,1200 Brussels, Belgium

E-mail : latu@acp.int.
Mwisho wa kutuma  Agosti 31, 2012

Imetolewa na;

Ghonche Materego

Katibu Mtendaji - BASATA