Thursday, September 27, 2012

SIKU YA UTALII TANZANIA NA DUNIANI

Kazi ya Sanaa Mji mkongwe MIKINDANI
Wanayama wakivuka mto huko Serengeti - Tanzania



Sanaa MIKINDANI - MTWARA

Faru weusi huko Ngorongoro - Tanzania





















Leo ni siku ya UTALII TANZANIA NA DUNIANI: Utalii ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya uchumi duniani. Kuna nchi kadhaa ambazo hutegemea tu uchumi kujiendesha na kuendelea kuwepo. Kikubwa ni uwekezaji wa makusudi na lazima katika sekta hiyo yenye uwezo wa kuzalisha ajira lukuki. Tanzania ina mali asili nyingi mno ambazo ni vivutio tosha vya utalii; moja ya mambo yanayoturudisha nyuma katika hili ni uwekezaji hafifu kwa watu wetu.

 Uwekezaji huu utazame kwa makini hasa aina ya elimu tuitoayo kwa wanafunzi wetu; kwa kuwa tuna vivutio vingi vya utalii basi tuwe na mitaala yenye kulenga utalii toka shule ya msingi. Shule zetu ziwe na michepuo yenye kuendana na mahitaji ya karne ya ishirini na moja. Kuwe na shule zenye kuangazia masomo ya sayansi na teknolojia yenye kujibu mahitaji ya moja kwa moja ya watu wetu. Tukirudi kwenye utaliii, shule na mitaala yenye kufunza huo utalii zianze mapema kufunza yaliyo ya lazima; uaminifu, ukarimu, lugha za kigeni, na mengine muhimu hiyo itasaidia kutumia vyema rasilimali na utajiri mkubwa tuliopatiwa na Mwenyezi Mungu, kinyume na hivyo tutaendelea kuwalaumu majirani waliojipanga kunufaisha jamii zao na hiyo nd'o hasa jukumu la serikali.    


Friday, September 21, 2012

Mashindano ya Hisabati, kemia, Fizikia, Jiografia n.k

Msaani Akitoa burudani kwa umma- Mashindano ya mavazi, mavazi sahihi- picha kwa hisani ya google?
Hapa duniani kila jamii ina aina fulani ya burudani na hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu. Hata hivyo maisha ya nchi na watu wake ili yaweze kwenda mbele na nchi kupiga hatua za kimaendeleo ni muhimu ikawekeza kwa kiasi kikubwa zaidi katika elimu. Elimu kama tuambiawavyo nd'o ufunguo wa maisha. Elimu ndio inaweza kuwaweka sawa, kwa kiasi fulani, watoto wa tajiri na wamasikini. Ni kupitia hiyo elimu ndo mambo mengi iwe ni burudani; muziki, mpira, urembo, sana ya mavazi, iwe ni mawasiliano, sheria, tiba, taja tasnia zote; zinahitaji elimu ili kufanya vyema zaidi.

Nchini Tanzania, nchi yangu hii, kwa maoni yangu naona elimu hatuipatii fursa ya kutosha; ni kweli Serikali na wadau wengine wengi wanajitahidi kwa kiasi kikubwa kutoa huduma hiyo muhimu kwa jamii. Hata hivyo juhudi mara dufu bado yahitajika. Kuna njia na mbinu nyingi elimu inaweza kuiga toka kwenye kada nyingine hapa nchini.

Kwenye Muziki, filamu na sekta nyingine, wadau kadhaa wameanzisha tamasha maalumu kutafuta vijana wenye vipaji, na tamasha hizo zinafanywa kwa mbwembwe,ubunifu na bila shaka udhamini mkubwa na wenye gharama kubwa tu. Jambo hili ni jema sana kwani shughuli hizi zinachangia kuwakwamua vijana toka kwenye kukosa ajira na kuweza kupata kipato ambacho bila shughuli hizo wasingekipata.  Hata hivyo wazo na wito wangu: kuibuke wadau wengine watakao fanya mashindano ya vijana kwenye hisabati, fizikia, baiolojia, jiografia, kiswahili... wazunguke mkoa mmoja hadi mwingine kupata wataalamu wa hisabati, na kadhalika. Kufanya hivyo kutatuwezesha kupata teknolojia na kujenga hamu ya kubobea na kujikita zaidi  katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.