Monday, May 24, 2010

Vijana

Tunapoongelea wajenga dunia ni lazima kuangalia makundi ya watu. Kufanya hivyo hakumaanishi kuwa tunafanya ubaguzi. Kama ni lazima kuita kitu ubaguzi basi huu ni ule wenye nia na malengo mazuri.

Kwenye maendeleo binafsi huwapatia vijana nafasi  ya kipekee kabisa. Naamini kuwa kundi hili la wanadamu wana mengi ya kuchangia katika maendeleo ya jamii. Vijana wana nguvu, wana malengo mengi na mara nyingi makubwa na wengi wao wana ujasiri na uthubutu. Mambo haya muhimu yakijumuishwa na elimu inayowaelekeza vyema wana nafasi kubwa ya kufanya makubwa kwa jamii zao na kwa jamii ya wanadamu na dunia kwa ujumla wake.

Hali hii na hatua hii ya maisha, ukiacha ile ya utoto ambayo kila mwanadamu lazima aipitie, ujana ni hatua ya pili ambayo hupitiwa na wanadamu wengi zaidi kuliko ya utu uzima na ya uzee. Hatua ya utoto ndiyo ambayo wanadamu wote hupitia lakini hatua hii ni ya kupokea tu wala hakuna kutoa. Ni wazi kuwa watoto ni muhimu wapokee ili waweze kujengeka vyema na hatimaye wawe vijana, watu wazima na wazee wenye manufaa kwa dunia.

 Nakukaribisha kulielezea kundi hili la pili katika hatua za ubinadamu ili kuona mchango wake katika mapinduzi ya dunia.

Martin Mandalu